Wakati Tanzania ikithibitisha uwepo wa virusi vya Marburg, fahamu namna sahihi ya kujikinga

Wakati Tanzania ikithibitisha uwepo wa virusi vya Marburg, fahamu namna sahihi ya kujikinga

Watu 5 akiwemo mhudumu wa afya wamefariki na 3 wanapokea matibabu.
Tanzania flag and stethoscope I getty Images

Watu watano wamekufa nchini Tanzania kutokana na ugonjwa wa virusi vya Marburg kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo katika mkoa wa Kagera kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu alisema Jumanne tarehe 22.

Mwalimu alisema matokeo yao ya maabara ya afya ya umma yamethibitisha ugonjwa huo na kwamba mamlaka za afya zimefanikiwa kudhibiti kuenea kwake. lilisema

Visa vya awali vya maambukizi ya virusi vya Marburg nchini vilithibitishwa baada ya mamlaka ya afya ya Tanzania kufanya uchunguzi wa kimaabara juu ya ugonjwa wa ajabu ulioripotiwa athiri watu nane/

“Marburg ni kirusi kilochugundulika kwa mara ya kwanza kijiji cha Marburg nchini Ujerumani na ikapewa hio jina mwaka 1967.” Anafafanua Dkt Edesio Henry Makaria, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mikrobiolojia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nchini Tanzania, nchi ambako mlipuko huo ulitokea.

Virusi hivyo vilitoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu na kuna uwezekano mkubwa kuwa wanadamu ambao huingiliana na kujichanganya na wanyama huko vijijini.

Majimaji ya mwili ndio njia rahisi zaidi ya virusi kuenea mfano kama mate au ngono isiyo salama. Pia kupitia nyuso na nyenzo.

Kipindi cha ugonjwa kukaa ndani ya mwili ni kutoka siku ya pili ya kuambukizwa hadi siku ya 21 japo Wagonjwa wengi hupata dalili kali za kuvuja damu ndani ya siku saba mpaka tisa kutokana na milipuko ya nyuma, na hakuna chanjo wala tiba mpaka sasa.

“Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Marburg huanza ghafla, na homa kali, maumivu ya kichwa kali na uchovu wa hali ya juu.” Dkt Makaria aelezea TRT Afrika na kuongeza “Ugonjwa wa virusi vya Marburg, ambao uko katika familia moja na virusi vinavyosababisha Ebola, na kuuwa aidi, ni ugonjwa hatari sana unaosababisha homa ya hemorrhagic, na uwiano wa vifo vya hadi 90%.”

Dr Makaria anasisitiza kwamba watu watoe taarifa katika vituo vya afya vilivyopo karibu pindi wanapoanza kuona dalili kutoka kwa mgonjwa.

“Msijitibu nyumbani!” anaongeza Makaria

Virusi hupitishwa kwa watu kutoka kwa popo wa matunda na wanyama pori wanaoliwa katika maeneo hayo.

WHO imesema inaisaidia Wizara ya Afya ya nchi hiyo kupeleka timu ya dharura mkoani Kagera kufanya uchunguzi zaidi wa magonjwa ya mlipuko.

Mkurugenzi wa Africa CDC, Dr Ahmed Ogwell, kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema taasisi hiyo itashirikiana na Tanzania.

“Tuko pamoja na Tanzania katika mlipuko huu wa ugonjwa wa virusi vya Marburg. Africa CDC inatuma mara moja wataalamu ili kuimarisha Wizara ya afya ya Tanzania kukabiliana na kupunguza hatari za kuenea kwa Marburg.”

Ni namna gani unaweza ukajikinga?

Kulingana na ushauri wa Dkt Edesio Henry Makaria, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mikrobiolojia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nchini Tanzania, kuna njia kadhaa za kujikinga na kuambukizwa

Hapa ni chache zilizopendekezwa :

  • Kuvaa vazi ya kujikinga
  • Glavu na barakoa
  • Kuweka mtu aliyeambukizwa katika karantini au atengwe kabisa
  • Kuzingatia usafi au utupaji ipasavyo wa sindano, vifaa, na aina yoyote majimaji inayotoka kwa mwili wa mgonjwa - kama vile kinyesi, damu au mate

Kwa upande wa Afrika, mlipuko wa ugonjwa huu uliripotiwa kwa mara ya kwanza nchini Equatorial Guinea tarehe 7 Februari 2023 na tarehe 13 Februari 2023, ulitambuliwa kuwa ugonjwa wa virusi vya Marburg.

TRT Afrika na mashirika ya habari