Wafanyabiashara wamefunga duka zao Kampala na miji mingine jirani kama ishara ya maandamano kupinga mfumo mpya wa malipo wa URA / picha Kutoka UBC

Wafanyabiashara wamefunga maduka yao kwa kile wanachoita mfumo usio wa haki wa ushuru uliotolewa na Mamlaka ya Ushuru ya Uganda, URA.

Mfumo huu unaitwa Electronic Fiscal Receipting and Invoicing Solution (EFRIS).

"Tunagoma na kuandamana kwa amani ili kuonyesha kutoridhishwa na ongezeko la kodi. Kwa sasa, Mukono, Mbale, Kampala, Masaka, na Luweero wanashiriki kikamilifu, na tunatoa wito kwa mikoa mingine kuungana nasi katika mgomo huu," - Abdul Hakim Katongole, mwanachama wa Muungano wa wafanyabiashara wa Kampala, KACITA alisema.

Kato Mayanja, mfanyabiashara mjini Kampala alilalamikia mfumo huu mpya wa ushuru umewekwa kwa mauzo yenye thamani ya $39, 000 (150 mln UGSH) lakini anaelezea kuwa ingelenga katika mauzo ya thamani ya $260,000 (1 bln UGSH).

EFRIS iliyoanzishwa 2021 awali ilikuwa ikiwalenga kwa wazalishaji wakubwa na baadaye kupanuliwa na kujumuisha maduka makubwa na biashara kubwa.

Uliundwa ili kudhibiti ukwepaji kodi kwa kuboresha usahihi wa miamala iliyorekodiwa na kuhakikisha ulinganifu wa ushuru wa pembejeo na mazao, na hivyo kuongeza uwiano wa kodi kwa Pato la Taifa. .

Lakini Mamlaka ya Ushuru Uganda, URA inakana kuwa EFRIS si mfumo wa kutoza Ushuru.

"EFRIS ni mfumo unaowawezesha waendeshaji biashara kufanya miamala na kudhibiti utoaji wa risiti za kielektroniki na ankara za kielektroniki kwa wakati halisi. Kwa hivyo ni zana ya kisasa ambazo hurahisisha shughuli zote za biashara na usimamizi wao kila siku," URA imejitetea.

"EFRIS ni muhimu ili kubadilisha mfumo wa uchumi wa nchi yetu. Biashara lazima ziwe na uwezo wa kuzoea mazingira mapya ya udhibiti, kama zinavyofanya na mabadiliko ya teknolojia," anasema Mark Ruhindi ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ushuru.

Issa Ssekito, msemaji wa Muungano wa wafanyabiashara wa Kampala, KACITA anasema URA haijatimiza mfumo huo mpya kwa njia sahihi.

"Kama EFRIS ingetekelezwa na miongozo ambayo tulipewa, EFRIS hii isingekuwa inaleta matatizo kama ilivyo," Ssekito amewaambia vyombo vya habari.

Wafanyabiashara wanadai kuwa kiwango cha sasa cha ushuru kwa huduma na bidhaa ya 18%, kwa kila mfanyabiashara bidhaa zinapohamia kwa mfanyabiashara au biashara nyingine.

Wanadai ni sawa na ushuru mara mbili na hii inapunguza ushindani wao katika kanda hasa Kenya, ambayo VAT yake ni 16%.

TRT Afrika