Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov akiwa na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi Mei 29, 2023. PICHA/Facebook/Ikulu ya Kenya.

Katika taarifa ya pamoja ya Jumanne, Julai 18, 2023, mabalozi nchini Kenya walitoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ili kuepusha mipango ya kupinga serikali iliyopangwa kufanyika Jumatano, Alhamisi na Ijumaa.

"Tunasikitishwa na watu kupoteza maisha na tunasikitishwa na hali ya juu ya ghasia, ikiwa ni pamoja na utumiaji wa risasi za moto na uharibifu wa mali, wakati wa maandamano ya hivi majuzi.

Tunatambua hali ngumu ya kila siku inayowakabili Wakenya wengi na tunataka pande zote kuwasilisha wasiwasi wao kupitia mazungumzo ya maana na kusuluhisha tofauti zao kwa amani ili kujenga taifa kwa pamoja, bila kuhakikisha kupoteza maisha tena," sehemu ya taarifa iliyotolewa na wanadiplomasia wa Magharibi, wakiongozwa na Marekani na Uingereza, ilisema kupitia ukurasa wa Twitter.

Ubalozi wa Urusi nchini Kenya uliitikia taarifa ya pamoja iliyotolewa na wanadiplomasia wa Magharibi.

Urusi ilisema kauli ya wanadiplomasia wa nchi za Magharibi si chochote zaidi ya kuingilia masuala ya ndani ya Kenya.

"Ikiwa sio kuingiliwa katika mambo ya ndani, ni nini?" Ubalozi wa Urusi ulitweet.

TRT Afrika