Januari mwaka huu , Uganda ilizindua mpango wake wa kwanza wa kuchimba mafuta katika eneo la Kingfisher, chini ya Ziwa Albert Magharibi mwa nchi.
Serikali ya Uganda inasema iko tayari kupokea ombi kutoka kwa watoa mtaji wa sekta ya umma ili kushiriki katika mradi wa kujenga kiwanda cha kusafishia mafuta.
"Kuna idadi ya vipengele bora ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wa ufadhili wa mradi," wizara ya nishati na madini ya Uganda imesema katika taarifa, " na serikali ya Uganda sasa iko tayari kupokea ombi kutoka kwa watoa huduma wa mitaji ya kisekta ya umma ili kushiriki katika mradi huu wa kimkakati wa kitaifa na kikanda."
Uganda inatafuta ufadhili mpya baada ya mazungumzo na muungano uliojumuisha kitengo cha kampuni ya Marekani ya General Electric kushindikana.
Hii ni baada ya serikali kushindwa kutafuta fedha kwa wakati, wizara yake ya nishati na madini ilisema.
Kiwanda cha kusafisha mapipa 60,000 kwa siku kingegharimu wastani wa dola bilioni 3 hadi bilioni 4 na kusaidia nchi hiyo ya Afrika Mashariki kushughulikia akiba yake ghafi ambayo inatarajia kuanza kuzalisha mwaka 2025,
"Tuna shughuli za uchimbaji visima zinazoendelea, na pia tuna matumaini kwamba hivi karibuni tutafanya uvumbuzi mpya zaidi ili kuongeza msingi wa rasilimali za sasa," anasema Dkt. Jane Mulemwa, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Petroli ya Uganda.
Uganda ina nia ya kujenga bomba kubwa la kusafirisha mafuta ghafi kwenye masoko ya kimataifa kupitia bandari ya bahari ya Hindi nchini Tanzania.
Katika kilele, Uganda inapanga kuzalisha takriban mapipa 230,000 ya mafuta ghafi kwa siku.
Akiba ya mafuta ghafi nchini inakadiriwa kuwa mapipa bilioni 6.5, ambapo mapipa bilioni 1.4 yanaweza kurejeshwa.