Muda wa kuhesabu watu ulioanza tarehe Mei 10, 2024 ulitakiwa kumalizika rasmi Mei 19, 2024 lakini muda ukaongezwa hadi 25 Mei 2024 / Picha kutoka UBOS 

Shirika la Takwimu Uganda, UBOS limesema asilimia 99 ya watu walihesabiwa katika sensa ya watu na makazi kitaifa ya 2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa UBOS Dkt. Chris Mukiza amesema asilimia 1 pekee ndiyo iliyokosekana kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa wanakaya na watu wengine kukataa kushiriki.

"Tunafahamu baadhi ya maeneo ambayo yalirukwa kimakusudi na maafisa wa sensa. Tunapanga kurejea maeneo haya wiki hii na kuhesabu," Mukiza ameelezea waandishi wa habari.

Shirika hilo pia linasema kuwa linaanza kuandaa takwimu hizo na ripoti ya awali itakayotolewa tarehe 24 Juni, ripoti ya muda tarehe 24 Septemba na ripoti ya mwisho tarehe 24 Disemba 2024.

Muda wa kuhesabu watu ulioanza tarehe 10 Mei 2024 ulifaa kumalizika rasmi Mei 19, 2024.

Hata hivyo, maeneo ambayo hayakuanza tarehe 10 Mei 2024, kutokana na ugumu wa kufikiwa na mengine kutosajiliwa yaliruhusiwa kuhesabiwa hadi 25 Mei 2024.

Hii ni sensa ya sita ya watu kufanyika nchini Uganda tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1962. Kwa kawaida hufanyika baada ya kila miaka 10.

TRT Afrika