Uganda inaagiza kutoka nje kiasi kikubwa cha nguo zilizokwishatumika / Picha: AFP

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amepiga marufuku uingizaji wa nguo zilizokwisha tumika katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, akisema kuwa inakandamiza maendeleo ya viwanda vya nguo vya ndani na kwamba nguo hizo ni za watu wa Magharibi waliokufa.

Uganda inaagiza kutoka nje kiasi kikubwa cha nguo zilizokwishatumika, ambazo baadhi ya wateja wanapendelea kwa sababu ni za bei ya chini.

Lakini wazalishaji wa ndani wanalalamika kutupwa kwa nguo za mitumba kunaumiza soko, na kudhoofisha uwezo wa Uganda kupanda mnyororo wa thamani wa sekta ya pamba na nguo.

"Ni za watu waliokufa. Mzungu anapokufa, hukusanya nguo zao na kuzipeleka Afrika," Museveni alisema Ijumaa.

Nguo za msaada

Angalau 70% ya nguo zinazotolewa kama msaada barani Ulaya na Marekani huishia Afrika, kulingana na Oxfam, shirika la misaada la Uingereza.

Shirika la habari la Reuters halikuweza kubaini mara moja ni asilimia ngapi ya nguo zilizotolewa zilitoka kwa watu waliofariki.

"Tuna watu hapa ambao wanazalisha nguo mpya lakini hawawezi kujipenyeza sokoni," Museveni alisema katika hafla ya uwekaji msingi wa viwanda tisa katika eneo la Viwanda ya Sino-Uganda Mbale mjini Mbale.

"Tuna watu hapa ambao wanazalisha nguo mpya lakini hawawezi kujipenyeza sokoni," Museveni alisema katika hafla ya uwekaji msingi wa viwanda tisa katika Bustani ya Viwanda ya Sino-Uganda Mbale mjini Mbale.

Uganda ni mzalishaji mkubwa wa pamba lakini sehemu kubwa yake inauzwa nje ikiwa imesindikwa nusu nusu, na thamani ya mauzo yake ya pamba kati ya dola milioni 26-76 kwa mwaka, katika miaka kumi iliyopita 2022, kulingana na benki kuu ya Uganda.

Marufuku kamili

Jumuiya ya Afrika Mashariki, kikundi cha kiuchumi kikanda ambacho Uganda ni mwanachama, ilikubali mwaka 2016 kupiga marufuku kabisa uagizaji wa nguo zilizotumika ifikapo mwaka 2019, lakini Rwanda ndiyo nchi pekee iliyoidhinisha.

Kutokana na hali hiyo, Marekani mwaka wa 2018 ilisimamisha haki ya Rwanda ya kuuza nguo bila ushuru kwa Marekani, mojawapo ya manufaa ya mpangilio ya AGOA , yaani mpangilio ya ushuru wa Marekani kwa nchi za Afrika (AGOA).

Ubalozi wa Marekani mjini Kampala haukujibu mara moja ombi la barua pepe la kutaka maoni.

Museveni alisema marufuku hiyo pia itaenea hadi mita za umeme na nyaya za umeme, akisema zinafaa kununuliwa kutoka viwandani nchini Uganda.

TRT Afrika