Uganda imetenga sekta nne kama vyanzo vyake vya maendeleo ambazo ni kilimo, huduma, mawasiliano na teknolojia na viwanda.
Serikali sasa imeamua kuwekeza zaidi katika sekta ya mwasiliano na teknolojia kwa ajili ya kurahisisha maisha ya wananchi. Inapanga kuzindua marekebisho ya kidijitali.
"Kiini hasa cha ICT ni kuunda njia za muunganisho, ufanisi, na uwazi. Na wakati ulimwengu umekubali jukumu lake la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuwezesha mawasiliano, leo, tunaamini kuwa ICT ina nguvu ya kuokoa maisha," Dr. Amina Zawedde, Katibu Mkuu katika sekta ya mawasiliano na teknolojia ya Uganda aliambia waandishi wa habari.
Lakini je, mabadiliko yapi yanazingatiwa?
Kuongeza upenyezaji wa ICT kwa mtandao kutoka asilimia 25 hadi asilimia 50
Kufanya huduma za serikali kuwa rahisi mitandaoni,
Kupunguza gharama ya vifaa na huduma za ICT na gharama ya simu ya mkononi na ya kompyuta.
Kupunguza gharama ya vifaa na huduma za ICT kata bei ya data gharama ya simu ya mkononi na gharama ya kompyuta
Kurahisisha huduma za afya, elimu, huduma za umma, au ujasiriamali,
Kuunda kazi 30,000 za moja kwa moja kila mwaka ndani ya sekta ya ICT