Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Kituuma Rusoke./Picha: Jeshi la Polisi Uganda

Vyombo vya usalama nchini Uganda vimefanikiwa kumuokoa Muhammad Ali Abdul Amidu, mwanadiplomasia wa Kimisri mikononi mwa watekaji.

Kulingana na Jeshi la Polisi la Uganda, Amidu alitekwa siku ya Novemba 8, huku watekaji hao wakitaka walipwe kiasi cha fedha.

“Watu hao walitishia kumuua mwanadiplomasia huyo kama sharti lao la kulipwa Dola za Kimarekani 40,000 lisingetimia,” ilisema taarifa ya Jeshi la Polisi la nchi hiyo.

Siku ya Jumatano, kikosi cha pamoja cha Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Polisi nchini Uganda, vilifuatilia mienendo ya watekaji hao na kufanikiwa kuwakamata katika eneo la Wakiso.

“Mmoja ya watekaji hao aliwauwa wakati wa makabiliano na vikosi vya ulinzi na usalama,” iliongeza taarifa hiyo.

TRT Afrika