Uganda imempata mfungwa mmoja na Mpox / Picha:  Huduma ya Magereza Uganda

Maambukizi ya Mpox yamepatikana katika jela ya Nakasongola katika eneo la kati la Uganda, msemaji wa Gereza hilo alisema Jumanne, akiongeza kuwa mgonjwa huyo alikuwa ametengwa na alikuwa akipokea matibabu.

Shirika la Afya Duniani lilitangaza mlipuko huo, ambao uligunduliwa kwa mara ya kwanza katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwanzoni mwa mwaka, na baada kutangazwa kwa hali ya dharura ya afya ya umma ya kimataifa mwezi Agosti.

"Kwa bahati mbaya mfungwa huyo hakuweza kupewa dhamana kwa vile anazuiliwa kwa mauaji," alisema Frank Baine, msemaji wa Jeshi la Magereza Uganda. "Tunashuku aliingia na maambukizi lakini hilo linachunguzwa."

Takwimu za hivi punde zilizotolewa wiki iliyopita zilionyesha kwamba idadi ya maambukizi ya Mpox nchini Uganda imeongezeka na kufikia wagonjwa 41 nchini humo.

Msemaji wa Wizara ya Afya Emmanuel Ainebyoona alisema atatoa taarifa kuhusu mlipuko huo baadaye hii leo.

TRT Afrika