Muda rasmi ya sensa ya taifa nchini Uganda umekamilika.
"Muda wa kuhesabu watu na makazi ulioanza tarehe Mei 10, 2024 umemalizika mwishoni mwa siku, tarehe 19 Mei 2024. Hata hivyo, maeneo ambayo hayakuanza tarehe 10 Mei 2024, kutokana na ugumu wa kuingia na maeneo ya kuhesabiwa ambayo hayajasajiliwa kwenye mfumo, wanapewa fursa ya kuendelea kuhesabu," Shirika la Takwimu la Uganda, UBOS.
Siku ya kuhesabiwa imeongezwa hadi tarehe 25 Mei kwa ajili ya wale ambao hawakuweza kuhesabiwa.
"Iwapo hukupata nafasi ya kuwa sehemu ya Sensa ya Uganda 2024. Bado kuna fursa kwako. Wasiliana na maafisa wa baraza lako la mtaa ili kupanga kikao cha sensa," UBOS imesema katika taarifa.
Watu wote ambao hawajaorodheshwa wameombwa kuwasiliana na viongozi wao wa halmashauri kufanya miadi inayoonyesha ni lini watapatikana kuhesabiwa.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UBOS Dk. Godfrey Nabong anasema walifanikiwa kufikia kaya milioni 10.4.
Kwa mara ya kwanza hesabu ya idadi ya watu ilifanywa kwa njia ya kidijitali.
UBOS imesema matokeo ya sensa ya kiteknolojia yatatoka mwezi Juni 2024, matokeo ya muda kuwasilishwa Septemba 2024 na matokeo ya mwisho Disemba 2024.
Sensa ya 2024 itakuwa zoezi la sita kufanyika tangu Uganda kupata uhuru mwaka 1962.
I