Serikali ya Uganda imezindua mkakati wa uuzaji wa vanilla zaidi. / picha TRT Afrika

Wazalishaji wa zao la vanilla wanawataka wadau kuongeza mikakati ya mauzo, kuweka chapa na kuzingatia ubora, ili kuhifadhi nafasi ya Uganda katika soko la nje.

Serikali ya Uganda imezindua mkakati wa uuzaji wa vanila zaidi.

"Wakulima wa vanilla hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu hali ya kiuchumi ya Vanilla kwa sasa! Kila kitu kitarekebishwa. Wakulima tuwe na subira kidogo,” amesema mzalisha wa vanila nchini Uganda, kyakulaga Fred Bwino.

Baada ya kupaa hadi nafasi ya pili katika mauzo ya vanila barani Afrika, sekta hiyo imekua kwa kiasi kikubwa kutokana licha ya mwanzo wake duni.

Hata hivyo, wakulima katika wa sekta hii wanakabiliwa na changamoto kama kutokuwa na uhakika wa uzalishaji, hii inawafanya kutojua kupangia matarajio ya faida ya zao hili.

Kulingana na Benki Kuu ya Uganda, mwaka 2023 Uganda iliuza zaidi ya tani 189 ya vanila nje ya nchi, yenye thamani ya takriban dola milioni 20.

Makadirio ya serikali sasa yanaonyesha kuwa nchi inaweza kupata kati ya dola milioni 24 hadi 29 iwapo hali ya soko itakuwa shwari.

Lakini changamoto kubwa ya mauzo kwenda nje ni Uganda kusimamishwa kutoka katika mradi wa biashara na Marekani wa AGOA.

Marekani iliiondoa Uganda katika Mkataba wa Fursa ya Ukuaji wa Afrika (AGOA) kuanzia Januari 2024.

AGOA ambayo Iliyozinduliwa mwaka wa 2000, Sheria hiyo inatoa fursa kwa mauzo ya nje kutoka nchi za Kiafrika kupata soko la Marekani bila kutozwa ushuru.

Suala hili linawapa wakulima na wajasiriamali wa Uganda wasiwasi wa bidhaa zao.

"Pamoja na msamaha wa kutotozwa ushuru katika miezi michache mingine, wateja wetu watalazimika kununua vanila kwa bei ya juu," anasema Simon Musisi. "Kwa kawaida, watachagua kuagiza bidhaa kutoka Madagascar, ambayo bado iko chini ya AGOA. Tutaathirika vibaya."

Musisi, amekuwa akisafirisha tani 80 za vanila kila mwaka kwenda Marekani, na kupata dola za Marekani milioni 2.

Seriklai inasema kuwa ikitimiza mkatati wake wa mauzo vizuri basi wakulima wa vanila hawatakuwa na cha kuogopa, watapata mapato zaidi.

TRT Afrika