Kupimwa Hepatitis nchini Uganda ni bure/ picha kutoka WHO

Kupimwa Hepatitis nchini Uganda ni bure.

Shirika la Afya duniani linasema virusi vinavyoshambulia ini vinaweza kusababisha maambukizo ya ini, saratani ya ini, kushindwa kwa ini, na kifo.

Mnamo mwaka wa 2022, inakadiriwa kuwa wananchi 1250, nchini Uganda walikufa kwa ugonjwa huo, na karibu 6% ya watu wa Uganda bado wameambukizwa kwa muda mrefu.

Kulingana na ripoti ya takwimu ya wizara ya afya ya Uganda kiwango cha maambukizi ya Hepatitis B kati ya watu wazima wenye umri wa miaka 15-64 ni asili mia 4.1

Hata hivyo, maambukizi miongoni mwa wanaume ni ya juu kwa asilimia 5 na kwa wanawake ni asilimia 5.

"Madawa ya kulevya, matumizi ya pombe kupita kiasi ni kati ya vhanzo cha kuathirika kwa maini , " anaongezea Dkt. Beyagira, " wengine ni kwasababu ya madawa ya kienyeji ambayo hayafai. Lakini pia kuna madawa ya kawaida ambayo tunaununa kwa maduka ya dawa lakini ukitumia zadii ya inavyopasa inakuathiri .

Shirika la afya duniani, WHO, inasema ulimwenguni, 90% ya watu wanaoishi na virusi vya Hepatitis B na C hawajui kuwa wanayo, na hii inasababisha wastani wa vifo 3000 kila siku.

Ni muhimu kuelewa Hepatitis

Watu wazima walio na umri wa miaka 60 au zaidi bila sababu za hatari zinazojulikana za hepatitis B wanaweza pia kupokea chanjo ya hepatitis B.

Kenneth Kabagambe ameishi na hepatitis tangu 2012 na hapo ndipo akaanzisha shirika la kuangazia ugonjwa huu.

"Nilipopata ugonjwa huu wengi wa watu nchini Uganda hawakujua kuhusu ugonjwa huu, watu walidhani ni kwasababu ya uchawi na hata shida zingine ambazo hazikuambatana," anaelezea Kabagambe .

Kabagambe sasa ana shirika ambalo linaangazia ugonjwa huu.

"Wengi wa wagonjwa hawapati uchunguzi unaotakiwa kwa ajili ya kugundua na kututambua ikiwa wanahjitaji matibabu, vituo vingine vya uchunguzi vipo mbali sana na watu hawawezi kuzifikia kwa urahisi," Kabagambe anasema.

"Watu wengine wanaacha kuendelea kwenda kufuatailia hali yao kwa sababu wahudumu pia hawana uwezo wa kuwatafuta kila mara. Hapo sasa ndipo wagonjwa wanajipata katika mikono ya matabibu wa kinyeji ambao hawapi matibabu yanayofaa, kwasababu hawajui lolote kuhusu Hepatitis."

Kujikinga na Hepatitis

Chanjo ya hepatitis B inapatikana kwa watu wa rika zote.

Chanjo cha hepatitis B inapendekezwa kwa watoto wote wachanga, watoto wote au vijana walio na umri wa chini ya miaka 19 ambao hawajapata chanjo.

Watu wazima wote wenye umri wa miaka 19 hadi 59, na watu wazima wenye umri wa miaka 60 au zaidi walio na sababu za hatari za maambukizi ya hepatitis B pia wanaweza kupata chanjo.

Shirika la Africa la CDC linapendekezwa kuwa chanjo ya kawaida ya homa ya ini kwa watoto wote wachanga inayoanza na dozi ya kwanza ndani ya saa 24 baada ya kuzaliwa (dozi ya kuzaliwa ya hepatitis B au HepB-BD) na dozi mbili au tatu za ziada ili kukamilisha mfululizo wa chanjo ya watoto wachanga ni muhimu.

TRT Afrika