Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda wanatishia kufanya mgomo huku mwaka wa masomo wa 2023/2024 ukikaribia kuanza.
Chuo kikuu cha Makerere ni chuo cha serikali.
Wanadai kuwa wanataka mahakama ya rufaa ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu irejeshwa kazini mara moja.
Baraza la Chuo kikuu hicho kilisimamisha operesheni ya mahakama ya rufaa ya watoa huduma wa chuo hicho kikuu, kwa takribani miezi minne sasa ikidai kuwa haikuundwa ipasavyo kutokana na kuwa mwenyekiti wake Jaji Patrick Tabaro kukosa sifa stahiki.
Kutokuwepo kwa mahakama hii ya rufaa kunaondoa njia muhimu ya kutafuta haki katika kesi za kufukuzwa kazi.
Mahakama hiyo ya kihistoria imetoa jukwaa kwa wafanyikazi walioachishwa kazi kupinga maamuzi yaliyotolewa na bodi ya teuzi na kuhakikisha wanapata haki.
Kati ya malalamishi ya wafanyikazi ni kuwa kumekwa na ucheleweshwa wa kupandishwa vyeo kwa watumishi ambao wamemaliza PhD zao lakini hawajapandishwa ngazi ya kuwa wahadhiri.
Serikali ya Uganda ilitoa zaidi ya dola laki sita, katika mwaka wa fedha uliopita, ambazo ziliwezesha kutumia kuwapandisha madaraja wahadhiri 50.
Hata hivyo bado kuna upungufu wa angalau zaidi ya dola laki mia nne hamsini kuwapandisha vyeo watumishi wote wanaosubiri kupandishwa vyeo.