Mnamo Julai 28, wanakijiji walishtushwa na mabaki ya binadamu, ambayo polisi wakati huo walisema ni pamoja na mafuvu 3 ya watoto. / Picha: AFP

Polisi wa Uganda wamemkamata mwanamume mmoja kufuatia ugunduzi mbaya mwezi uliopita wa mafuvu 17 ya vichwa vya binadamu kupatikana katika kaburi moja magharibi mwa mji mkuu Kampala, maafisa walisema Jumanne.

Mnamo Julai 28, wanakijiji walioshtuka walishuhudia mabaki hayo, ambayo polisi wakati huo walisema ni pamoja na mafuvu matatu ya watoto, katika chumba kilichoko chini ya ardhi katika mji wa Mpigi, uliopo kilomita 30 (maili 18) magharibi mwa Kampala.

"Kikosi cha polisi cha upelelezi wa uhalifu kilipata taarifa na wakamkamata Lujja Bbosa Tabula mnamo Agosti 19," msemaji wa polisi Kituuma Rusoke aliambia AFP Jumanne, akisema yupo kizuizini.

“Tabula alikuwa akitafutwa kuhusiana na mafuvu ya vichwa vya binadamu viliyokutwa katika makazi yake huko Mpigi hivi karibuni,” alisema.

Kesi nyingine ya mauaji

Rusoke alisema Tabula atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika. Hajaweka wazi tarehe ya kufikishwa mahakamani.

Bado haijulikani jinsi mafuvu ya kichwa yaliishia sehemu hio, iliyoko kwenye juu ya mlima, na iliyozikwa ndani ya masanduku manne ya chuma ndani ya chumba kilicho chini ya ardhi kwa undani wa mita mbili (futi saba).

Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti wakazi wakisema kwamba watu walikuwa wamekusanyika hapo awali kuabudu.

Tabula pia alikuwa akitafutwa na polisi kuhusiana na kesi tofauti inayohusu mauaji ya kiongozi maarufu wa kimila wa Baganda, mjasiriamali Daniel Bbosa, na alikuwa akitoroka kabla ya kugunduliwa kwa mafuvu hayo.

Mauaji hayo mjini Kampala yaliripotiwa kutekelezwa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wakati Bbosa akirejea nyumbani kutoka kazini Februari mwaka huu.

TRT Afrika