Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kuwa zaidi ya wapiganaji 567 wanaohusishwa na kundi la kigaidi la Daesh wameuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia oparesheni ya wanajeshi wake nchini humo.
Baada ya kupata kibali cha Kongo, wanajeshi wa Uganda walianzisha operesheni huko dhidi ya ADF wakitaka kuharibu kambi zao na kuua au kuwakamata wapiganaji wa kundi hilo.
Katika hotuba yake Alhamisi jioni Museveni alisema wapiganaji 567 wa ADF wameuawa na wengine 50 kukamatwa. Alisema bunduki ndogo na maguruneti ya roketi ni kati ya vipande 167 vya vifaa vilivyopatikana kutoka kwa waasi.
"Wanatapatapa sasa ... chaguo pekee kwao ni kujisalimisha," Museveni alisema.
Kundi la kigaidi linalofanya mashambulio ya mara kwa mara nchini Uganda Allied Democratic Forces (ADF) liko katika misitu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako linaanzisha mashambulizi ndani ya Kongo na Uganda.
Museveni aliwataka waendeshaji wa mabasi, masoko na hoteli nchini Uganda kuwa waangalifu na kusajili wateja wote ili kuzuia washambuliaji wanaowezekana wa ADF kutumia vifaa vyao.