Wanajeshi wa Uganda wakiwa Somalia/ AFP  Tina SMOLE

Zaidi ya wanajeshi 6,000 wa Uganda walitumwa nchini Somalia tangu mwaka 2007 kusaidia mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la al-Shabab.

Lakini uamuzi huu wa sasa umetangazwa kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Abubaker Jeje Odongo.

Alisisitiza kuwa Uganda inaunga mkono amani, usalama na utulivu wa Somalia.

"Uganda ni nchi ya kwanza kupeleka wanajeshi na kuchangia amani nchini Somalia," alisema.

Abubaker Jeje Odongo alisema kuwa wanajeshi 2,900 wa Somalia wamepewa mafunzo na jeshi la Uganda , akaongeza kuwa wanajeshi 3,000 wa Somalia wanaendelea na mafunzo yao kama sehemu ya juhudi za kuunda vikosi vya SNA kuchukua majukumu ya usalama baada ya wao kuondoka,"

Hata hivyo Waziri huyo alisema pamoja na mafanikio ya AMISOM/ATMIS, baadhi ya changamoto za kiusalama zinazojirudia mara kwa mara ambazo zinatishia mafanikio hadi sasa huku akitoa wito wa kuwepo kwa ulinzi wa nguvu ambao ni pamoja na utoaji wa viongeza nguvu na viwezeshaji.

Aliwakumbusha wajumbe kwamba mpango wa mpito wa Somalia unatazamia kukabidhiwa majukumu ya usalama kwa Vikosi vya Usalama vya Somalia ifikapo Desemba, 2024.

TRT Afrika na mashirika ya habari