Serikali ya Uganda inapigana na ufisadi katika sekta ya umma  / Picha kutoka Parliament Watch

Serikali imepiga marufuku ajira yoyote ya wafanyakazi wapya katika mwaka wa Fedha wa 2024/25, isipokuwa kama idhini ya wazi imetolewa na Wizara ya Fedha na Wizara ya Utumishi wa Umma.

Tangazo hilo lilitolewa na Ramathan Ggoobi, Katibu wa Hazina katika Waraka wa Utekelezaji wa Bajeti wa Julai 2024, ambao ulitolewa ili kuongoza mashirika kuhusu jinsi ya kutekeleza na kusimamia bajeti ya taifa ya 2024/25.

“Hakutakuwa na ajira ya watumishi (utumishi wa umma au wafanyakazi wa kandarasi) katika mwaka wa fedha isipokuwa kwa msingi maalumu, kwa mfano ikiwa mfanyakazi mwengine ameachia nafasi yake ya kazi, ikiwa mtu hana uwezo wa kufanya kazi aliyoapewa, na ambapo fedha zimetolewa kwa ajili ya kuajiri walimu na wafanyakazi wa afya," Ngobi aliongezea.

"Pia kukiwa na kibali cha wazi kutoka Wizara ya Fedha pamoja na ile ya Utumishi wa Umma. Maafisa ( accounting officers) wanatakiwa kupata kibali kutoka kwa Wizara ya Utumishi wa Umma kabla ya kupata wafanyakazi wapya walioajiriwa kwenye orodha ya malipo,” aliandika Ggoobi.

Mnamo Februari 2022, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alifanya uhakiki wa kitaifa wa mishahara ya Serikali kwa kipindi cha miaka minne ya fedha 2019/20 hadi 2022/23.

Alipendekeza kurejeshwa kwa Sh53Bn ($14,227,198) kutoka kwa "watumishi hewa" 10,192 waliokuwa wakichota mishahara kutoka vyombo mbalimbali vya Serikali, baada ya baadhi kubainika kufariki, kustaafu au kutoroka kazini.

Ggoobi aliwataka maafisa kuhakikisha watumishi wa Serikali wa sasa na wajao wanapata orodha ya mishahara tu baada ya kutengeneza nyaraka kadhaa zikiwemo;

Nambari ya Kitambulisho cha Taifa (NIN), Nambari ya Utambulisho wa Ushuru (TIN), Nambari ya Mgavi wa IFMS na Mfumo Jumuishi wa Watumishi na Mishahara (IPPS)/Nambari ya Usimamizi wa Rasilimali Watu.

TRT Afrika