Reli hiyo itakarabatiwa kwa utaalamu wa kampuni ya China Road and Bridge japo kwa gharama ya serikali ya Uganda. / Picha: Reuters

Uganda imeanza kufanyia ukarabati sehemu ya njia ya reli iliyojengwa takriban karne moja iliyopita kwa matarajio kuwa itakupunguza gharama ya usafirishaji wa bidhaa kaskazini mwa nchi hiyo, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, msemaji wa shirika la reli alisema.

"Lengo letu ni kuhamisha usafirishaji wa mizigo ya masafa marefu kwenye reli kutoka barabarani katika miaka michache kwa sababu reli ni ya bei nafuu kwa gharama na wakati," John Linnon Sengendo, msemaji wa Shirika la Reli la Uganda (URC) aliiambia shirika la Reuters.

Uganda iliamua kufufua mtandao wa zamani wa reli baada ya mipango ya kujenga reli mpya ya kisasa ya standard gauge (SGR) kushindwa kupata ufadhili kutoka China.

Reli hiyo ya kale ambayo haijatumika kwa takriban miaka 40, ni sehemu ya mtandao wa reli wa Afrika Mashariki unaoanzia Mombasa, Mji wa Pwnai ya Kenya karibu na Bahari Hindi hadi kupasua Uganda na kufikia Kaskazini mwa nchi hiyo.

Ilijengwa na Utawala wa kikolonoi wa Uingereza karibu na mwanzo wa karne ya 20.

Hata hivyo bado reli hiyo itakarabatiwa kwa utaalamu wa kampuni ya China Road and Bridge japo kwa gharama ya serikali ya Uganda.

Sehemu ya kilomita 382 ya reli hiyo itakayokarabatiwa inaunganisha mji wa Tororo Mashariki mwa Uganda karibu na mpaka na Kenya na kuishia katika kituo cha usafirishaji huko Gulu kaskazini mwa Uganda karibu na mpaka na Sudan Kusini.

TRT Afrika
Reuters