Kamati ya Bunge la Utalii, Biashara na Viwanda imeanza kuchunguza madai ya ubadhirifu wa fedha za serikali iliyotolewa kwa vyama vya ushirika.
Kamati hiyo ilibaini kuwa tangu mwaka 2018, Sh5 bilioni pekee kati ya Sh15.5 bilioni ndizo zilizopokelewa, na kuziacha zilizosalia kutiwa kapuni na kampuni mbili za uwakili, Matovu & Matovu Company Advocates na Makada Company Advocates.
Aidha, Wabunge hao walisikitishwa baada ya kujua kwamba vyama vya ushirika vilifanya kazi kwa Mkataba wa Maelewano na makampuni ya sheria, ili kubakia na asilimia 40 ya jumla ya fedha za fidia ambazo makampuni hayakuwahi kuheshimu.
Hayo yamebainika wakati kamati hiyo ikiongozwa na Mbunge Mwine Mpaka, ilianza uchunguzi wake katika Wilaya ya Jinja, mashariki mwa Uganda, ambako walikutana na mashirika ya Busoga Growers Cooperative (BGC) na Jinja Multipurpose Cooperative Society (JMCS), walionufaika na fidia ya hasara ya vita Jumatatu, 04 Septemba 2023.
Kamati hiyo inatarajiwa kuendelea na uchunguzi wake katika wilaya za Mbale, Soroti, Lira, Gulu, Masindi na Nakaseke.