Serikali ya Uganda imepoteza takribani Ush 392 bilioni sawa na $96.2 milioni katika kipindi cha miaka mitano iliyopita katika ada za ahadi zilizolipwa kwa mikopo ambayo haijatumika.
Ada ya ahadi ya mkopo ni kiasi cha pesa kinacho tozwa na mkopeshaji ili kuweka mkopo mahususi upatikane.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, John Muwanga, alisema katika ripoti yake ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 2022 kuwa pesa kiasi cha USh15.6 trilioni, dola bilioni 4.2, zilikopwa na serikali, lakini fedha hizo bado hazijatolewa, na hivyo kukaribisha mchakato wa ada za mikopo.
"Kushindwa kwa serikali kupunguza na uchukuaji mdogo wa deni la serikali iliyoingia mkataba kunaendelea kuvutia ada kubwa za ahadi na kuathiri utoaji wa huduma," Muwanga alisema katika ripoti hiyo iliyonukuliwa na Daily Monitor.
Mikopo mingi ambayo haijalipwa ilichukuliwa kujenga barabara, mitambo ya kuzalisha umeme kwa maji na miradi mingine ya maendeleo.
Kwa mfano, mradi wa Kampala-Jinja Expressway ulipaswa kufadhiliwa kupitia mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, ADB, wa Ush842 bilioni sawa na dola $225.5 milioni.
Deni lilikuwa limepatikana lakini halikuchukuliwa, na kugharimu Ush3.97 bilioni (dola milioni 1.1) kama ada ya ahadi, mkaguzi mkuu alisema.