Maji ya mafuriko yameathiri nchi kadhaa Afrika Mashariki, mwanzoni mwa mwezi wa Mei. / Picha: Reuters

Na

Firmain Eric Mbadinga

"Hasira ya asili", sitiari inayotumika mara kwa mara kwa matokeo ya matendo ya binadamu ambayo huathiri vibaya sayari, imejidhihirisha hivi majuzi katika mfululizo wa majanga ya hali ya hewa - kutoka kwa mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi barani Afrika, ambayo yaliua au kuwahamisha maelfu ya watu wakati huko Dubai mvua ya miezi 18 iliyonyesha katika masaa 24.

Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda, Somalia na Ethiopia zote zimekumbwa na maafa ya mafuriko na maporomoko ya ardhi katika bara hilo katika miezi ya hivi karibuni, na kusababisha wanasayansi kubaini mabadiliko ya hali ya hewa kama sababu kuu ya maafa haya ya mara kwa mara.

Maji ya mafuriko yalipoanza kupungua, dhoruba ya Kimpunga Hidaya ilipiga pwani ya Kenya na Tanzania mnamo Mei 4, na kusababisha masaibu zaidi kwa majirani wa Afrika Mashariki. Kimbunga hicho kiligharimu maisha ya watu 400 na kusababisha uharibifu wa mali unaokadiriwa kufikia dola milioni kadhaa.

Kwa hivyo, ni nini ambacho sayansi inalenga kufanya, sio tu kuzuia athari za matukio yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini katika kufaidika na maji na nishati?

Ingawa inaweza kutoaminika, huu ni msururu wa mawazo ya kisayansi kwani janga moja la asili baada ya lingine husukuma sehemu fulani ya sayari kila baada ya miezi michache.

Mafuriko yaliyotokea Afrika Mashariki yalikuwa mabaya zaidi kwa miongo kadhaa. / Picha: Reuters

Mikakati ya ubunifu

Wataalamu wanahusisha mvua kubwa na isiyo ya msimu katika sehemu za bara la Amerika Kusini na Afrika na El Niño.

"El Niño hutokea wakati maji ya Bahari ya Pasifiki yanakuwa na joto zaidi kuliko kawaida na upepo wa mashariki kupungua, na kusababisha joto la juu katika ulimwengu wa kaskazini na kuongezeka kwa mvua katika Amerika ya Kusini na kusini mwa Afrika," Dk George Mwaniki afananua, mkuu wa ubora wa hewa "WRI Afrika".

Ingawa El Niño na mambo mengine ya hali ya hewa yenye uharibifu yanaonekana kuwatesa wanadamu, tafiti za kisayansi zimetoa mbinu za kugeuza mvua kubwa na mawimbi ya joto kuwa vyanzo endelevu, vya maji na nishati.

Mbinu hizi zinakusudiwa kunasa maji na joto kupita kiasi, kama zile zinazoleta mvua kwenye jangwa.

Wanasayansi wana hakika kwamba tafiti na mbinu kama hizo zinaweza kuzuia majanga yanayohusiana na hali ya hewa na kusababisha usambazaji sawa wa rasilimali ulimwenguni kote.

Jovanie Sonie Ndong Songo, mbunifu na mpangaji miji nchini Gabon, anaamini kwamba mifumo sahihi ya ukuaji wa miji lazima ianzishwe katika kila nchi ya Afrika kabla ya teknolojia ya kukamata joto au maji kwa matumizi ya binadamu kubuniwa.

"Mbali na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, pia ni suala la matumizi endelevu ya ardhi na kuendeleza mbinu za kuzuia hatari. Maafa ya hivi majuzi nchini Kenya na mataifa mengine yameonyesha umuhimu wa kuwa na mifumo bora ya maji taka, mifereji ya maji na mifumo ya dharura," anaiambia TRT Afrika.

"Ni muhimu kufanya uvumbuzi katika muundo wa mitandao mipya inayojumuisha mabonde ya asili na ya kutengezeza ya kuhifadhi maji."

Mifano mengi ya kisayansi

Miundombinu ya kiufundi inayopendekezwa na Jovanie, pia inajulikana kama mabonde ya maji ya mvua, imeonyesha mafanikio katika nchi kama Canada. Baada ya mafuriko ya 2011 kusababisha Ziwa Champlain na Richelieu kufurika, utafiti ulipendekeza kuondolewa kwa mitaro yote.

Charlène Mouboulou, mwandishi wa habari na mhandisi wa mazingira, anapendekeza kwamba nchi zinaweza kuunda mabonde ya kuhifadhi au hata ziwa ya bandia, kulingana na eneo la jiografia, kutumia maji ya ziada.

"Maji kutoka kwenye mabonde haya yanaweza kutumika kwa ajili ya ujenzi, miradi ya umma, kilimo na ufugaji wa samaki, au hata majumbani. Sekta hizi zote zinahitaji maji mengi," anaiambia TRT Afrika.

Hassan Chouaouta, mwenzake kutoka Morocco na Rais wa Centre de Compétences pour la Durabilité (Kituo cha Ujuzi wa Maendeleo Endelevu), anasema mafuriko yoyote kutoka kwa mabonde wakati wa mvua kubwa kunaweza kutumika kuzalisha umeme.

"Tunaweza kuweka mpango mzuro kwa ya aina hii ya mafuriko. Ninaamini kuwa miji inahitaji kuwa na miundombinu imara ili kuzuia matokeo mabaya zaidi, lakini muhimu zaidi, kudhibiti na kuelekeza mafuriko kwenye mito au maeneo salama ambayo yanaweza kutumika kwa kuhifadhi maji," anasema Chouaouta.

"Tunaweza hata kuzalisha umeme wa maji na kutumia aina hii ya maafa kwa manufaa yetu."

Kabla ya mafuriko Somalia ilishuhudia ukame mbaya kutokea kwa miaka 40 ya nyuma. / Picha: Reuters

Kuunganisha mawimbi ya joto

Kabla ya mafuriko ya hivi karibuni, miezi ya kati ya 2023 ilipata mfululizo wa ongezeko la joto duniani, na kusababisha ukame katika baadhi ya maeneo na moto wa misitu katika maeneo mengine.

Katika jimbo la California la Marekani, zebaki ilifikia 54 ° C, na hivyo inawezekana kupika yayi halisi kwenye lami. Joto hilo pia lilisababisha vifo vya makumi ya watu.

Mnamo 2020, wakati mawimbi ya joto yalipoongezeka, Dk Mikael Philippe wa Ofisi ya Ufaransa ya Recherches Géologiques et Minières alikuwa tayari anazingatia nishati ya jotoardhi kama suluhisho la kupooza nyumba.

Dk Philippe anaelezea nishati ya jotoardhi kama "sayansi inayochunguza hali ya joto ya ndani ya ukoko wa Dunia na teknolojia inayolenga kuzitumia".

Mouboulou kwa mtazamo wake kuhusu suala la mabadiliko makubwa ya teknolojia ya jua. "Tunaweza kutumia nishati hii kutofautisha aina za kilimo. Baadhi ya maeneo hayawezi kuzalisha aina fulani za mazao kwa sababu ya hali ya hewa," anasema.

"Wazo ni kufanya joto isaliye kwenye jumba la kijani ili kupatikana kwa athari ya jumba la kijani kwa kiwango kidogo. Kwa njia hii, hatutahitaji mashine kuunda hali ya hewa ndogo ambayo inahimiza ukuaji wa aina kama vile zabibu na machungwa."

Katika maeneo yenye mvua chache, kupanda kwa mawingu ni chaguo pamoja na kupata maji kutoka maeneo yenye mvua nyingi.

Mbinu ya kisayansi ilibuniwa mnamo 1948 na Mmarekani Charles Mallory Hatfield, aliyepewa jina la "mwenye kutengeneza mvua". Inahusisha kueneza erosoli na chembe za barafu kwenye mawingu ili zijirundike na kugeuka kuwa mvua. Dubai imekuwa ikitumia mbinu hii kwa miaka mingi.

TRT Afrika