Jaribio hili la sasa kortini linatafuta fidia kwa wale wanaodai kuwa tayari wameumizwa kutokana na ujenzi wa mradi huo, ukosefu wa malipo kwa wakati kwa ardhi ambayo bomba litajengwa hadi nyumba zilizoharibiwa kutokana na mafuriko wakati wa ujenzi wa vituo vya kuchakata mafuta. Picha: Reuters

Makundi haya ya Ufaransa na Uganda, yakiongozwa na kundi la ‘Friends of the Earth France’, yanaishutumu kampuni hiyo ya nishati kwa kushindwa kulinda watu na mazingira kutokana na biashara yake ya mafuta na Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) lenye thamani ya dola bilioni 3.5.

Kesi yao inatumia sheria ya mwaka 2017 ya Ufaransa ya “wajibu wa kuwa macho” almaarufu a 2017 French "duty of vigilance" law inayohitaji makampuni makubwa kutambua na kudhibiti hatari katika shughuli zao za kibiashara.

“TotalEnergies inazingatia kuwa mpango wake wa umakini unatekelezwa ipasavyo na imehakikisha kuwa kampuni zake nchini Uganda na Tanzania zimetumia mipango ya utekelezaji ifaayo ili kuheshimu haki za jamii na viumbe hai,” msemaji wa kampuni hiyo ilisema kupitia barua pepe.

“Tunatazamia mjadala kuhusu uhalali mahakamani.”

Kampuni hiyo ina hisa 62% katika EACOP, ambayo ina urefu wa kilomita 1,443 (maili 897) kutoka maeneo ya mafuta ya Ziwa Albert nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania, ikiwa na uwezo wa kupeleka hadi mapipa 246,000 ya mafuta ghafi kwa siku katika soko la dunia kama vile mapema 2025.

Kesi ya kwanza ilitaka kusitisha miradi hiyo kwa amri ya mahakama chini ya mchakato maalum wa haraka, huku jaji akibainisha kampuni ya TotalEnergies ilikua imefanikisha iliyohitajika kufanyika kisheria.

Hukumu hiyo iliongeza hata hivyo kuwa uchunguzi wa kina pekee unaweza kuchunguza ikiwa hatua za kampuni hiyo mashinani ziliambatana na wajibu wake wa kuzuia madhara yanayoweza kutambulika.

Jaribio hili la sasa mahakamani linatafuta fidia kwa wale wanaodai kuwa tayari wameumizwa kutokana na ujenzi wa mradi huo, ukosefu wa malipo kwa wakati kwa ardhi ambayo bomba litajengwa hadi nyumba zilizoharibiwa kutokana na mafuriko wakati wa ujenzi wa vituo vya kuchakata mafuta.

TRT Afrika na mashirika ya habari