Waziri wa afya nchini Tanzania amesema kuwa tayari mmgonjwa mmoja aliyekuwa hospitali kwa maradhi ya marburg ameruhusiwa na anaendelea vizuri.
Hata hivyo waziri huyo amesisitiza kwa jamii ya watanzania kuto mtenga mgojwa wala kumnyanyapaa huku akiomba ushirikiano wa wananchi.
“Leo tumemruhusu mtu mmoja (Mwanaume wa miaka 26) aliyepona Ugonjwa wa Marburg, kurejea kwenye jamii. Ni matumaini yangu jamii itampokea na kushirikiana nae katika shughuli zake za kila siku" amesema Ummy Mwalimu
Waziri huyo amewahakikishia Watanzania na Jamii ya Kimataifa kuwa Tanzania ni salama hivyo wananchi waendelee na shughuli na safari bila hofu yeyote.
“Wananchi wote hasa wa Mkoa wa Kagera endeleeni kuchukua tahadhari kudhibiti ugonjwa na kuzuia maambukizi mapya katika jamii”
Katika kusisitiza hilo Waziri huyo wa afya Tanzania amethibitisha kuwa Tanzania haina wagonjwa wapya wa Marburg wala vifo. ni "jambo la kumshukuru Mungu kuwa hatujapata wagonjwa wapya wala vifo”
Wiki chache zilizo pita Tanzania ilithibitisha kuwa watu watano kati ya wanane walifariki dunia kutokana na ugonjwa wa virusi vya Marburg katika mkoa wa Kagera, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Kabla ya tanzania Marburg, kulizuka sintofahamu kubwa kutokana na kutajwa kuwa ni ugonjwa usiojulikana na baadhi walianza kuhusisha ugonjwa huo na ugonjwa wa ebola ulioua maelfu ya watu katika nchi jirani ya DRC.