Hatimaye washindi wa Tuzo za kila mwaka duniani maarufu, World Travel Awards wamejulikana huku Kenya na Tanzania wakifurahia ushindi wao katika vitengo mbalimbali.
Tuzo hizo maarufu za kusafiri ulimwenguni zimetangaza washindi wake wa mwaka huu wa 2023 kwa maeneo ya Afrika na Bahari ya Hindi, huku wakitambua chapa bora za kusafiri, utalii, na ukarimu katika mabara hayo.
Kenya ilitunukiwa tuzo ya eneo la kitalii linaloongoza bara Afrika 2023 na kuzipiku Botswana, Misri, Ghana, Malawi, Morocco, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Rwanda, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.
Aidha eneo la diani, lililoko sehemu ya pwani ya nchini Kenya pia limeshinda tuzo ya eneo lenye fukwe bora zaidi Afrika.
Shirika la ndege la Ethiopia, Ethiopia Airlines, ilishinda ndege inayoongoza afrika 2023.
Taifa la Tanzania lilizidi kutawala tuzo hizo kwani pia eneo la hifadhi la Ngorongoro, Tanzania lilijizolea kivutio kikuu cha utalii barani Afrika 2023.
Ngorongoro imeshinda tuzo hiyo baada ya kuvipiku vivutio vingine vya utalii barani Afrika kama vile table Mountain, Hartbeespoort aerial cableway, V& A Waterfront, Ruben Island vya afrika kusini, Ziwa Malawi, Okavango Delta ya Botswana, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Pyramis of Giza ya Misri.
Tuzo hiyo imepokelewa na Meneja wa huduma za Utalii NCAA Bw. Peter Makutian kwa niaba ya uongozi wa Shirika.
Bodi ya utalii ya Tanzania ndio mshindi wa taji la bodi Ya Utalii inayoongoza Afrika 2023
Wakatio huo huo, taji la hifadhi ya kitaifa inayoongoza afrika 2023, ilichukuliwa na hifadhi ya taifa ya Serengeti, Tanzania.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cape Town, Afrika Kusini umetunukiwa uwanja bora wa ndege afrika 2023.
Sherehe ya tuzo hizo za Kusafiri Ulimwenguni ilifanyika katika kituo kipya cha kihistoria cha Dubai, Atlantis Royal.