Kamishna wa uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania Profesa Dos Santos Dilayo amesema nchi inapoteza hekta 469,000 ya misitu kila mwaka / Picha:  Tanzania Forest Services Agency.

Tanzania imeanza mkakati wa kimataifa la kurejesha misitu kwa lengo la kuimarisha viumbe hai na kuboresha maisha.

Mpango huo unaofadhiliwa kwa dola milioni 4.5 (Sh12.15 bilioni), unalenga kurejesha hekta milioni 5.2 za misitu, kuashiria dhamira ya Tanzania katika Mpango wa Kurejesha Mazingira ya Misitu ya Afrika (AFR100), unaolenga kurejesha hekta milioni 100 za ardhi iliyoharibiwa nchini kote ifikapo 2030.

Mpango huo wa AFR100 unaongozwa na Mataifa ya Afrika na kusimamiwa na Shirika la Kimataifa la Mpango wa Urejesho wa Kimataifa ya Shirika la World Resource Institute, ambao ni mpango wa Umoja wa Mataifa wa kurudisha mfumo wa ikolojia.

Tanzania ilijiunga na mfumo wa AFR 100 mwaka 2018.

Kamishna wa uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania Profesa Dos Santos Dilayo amesema nchi inapoteza hekta 469,000 ya misitu kila mwaka.

Amesema ukataji wa misitu unatoa takribani tani milioni 43 ya hewa chafu ya 'carbondioxide' hewani.

"Misitu inachangia 3.9% katika pato la taifa la Tanzania ilihali inapata changamoto kubwa kwa wanaonyemelea kwa ajili ya kilimo, ukataji miti isiyo halali na mengineyo," amesema.

Bernard Urassa kutoka Ofisi ya Rais amesemea mradi huu unaofadhiliwa na Ujerumani pia unaipa Tanzania uwezo wa kupata faida ya biashara ya kaboni.

TRT Afrika