Sensa ya Watu na Makazi hufanyika kila baada ya miaka 10 nchini Tanzania./Picha: AFP  

Idadi ya Watanzania inatarajia kufikia milioni 140 ifikapo mwaka 2050, kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Benki ya Dunia.

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Tanzania nchini Tanzania, Nathan Belete amesema idadi ya watu inatarajiwa kuongezeka kila baada ya miaka 23.

Katika ripoti yake, Benki ya Dunia inasisitiza umuhimu wa kushughulikia ongezeko hilo huku kukiwa na uwezekano wa ongezeko la mahitaji muhimu ya jamii, baada ya idadi ya watu kuongezeka.

Kwa mujibu wa Belete, ongozeko la idadi ya watu Tanzania litakaua kwa asilimia tatu, kila baada ya miaka 23, na hivyo kuzipita nchi nyingine katika ukanda wa kusini wa jangwa la Sahara, ambao ukuaji wake ni asilimia 2.7.

Kwa sasa, idadi ya Watanzania imefikia milioni 61.7, kulingana na Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022.

Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Tanzania ilikuwa na idadi ya watu 44, 928, 923, hali inayoakisi ongezeko la watu 16, 812, 197, sawa na ongezeko la asilimia 3.2, ukilinganisha na mwaka 2012.

Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kukuasanya, kuchambua,kutathmini,kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalumu.

Zoezi hilo liliendeshwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mwaka 1910, huku michakato kama hiyo ikifuatia miaka ya 1967,1978,1988,2002 na 2012 baada ya uhuru.

TRT Afrika