Rais wa Somalia  Hassan Sheikh Mohamud amesema Ethipia ina uchokozi/ Picha: Wengine 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano kuhusu mvutano mpya kati ya Somalia na Ethiopia, Januari 17, mwaka huu.

"Baraza limekaribisha uamuzi wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika kumtuma mwakilishi mkuu wa AU wa pembe ya Afrika Olusegun Obasanjo kuhimiza maongezi kati ya nchi hizo mbili," ilisema taarifa yake.

Mkataba uliotiwa saini tarehe Januari, 1 mwaka huu kati ya Ethiopia na eneo la Somaliland utaiwezesha Ethiopia kukodisha kilomita 20 ya ukanda wa bahari kutoka Somaliland kwa ajili ya biashara zake na kuweka kambi ya majeshi hapo.

Kwa upande wake Ethiopia iliahidi kuitambua Somaliland kama nchi huru.

Somalia imesema haina nafasi ya kufanya makubaliano na Ethiopia kuhusu mvutano ambao umeifanya Somalia kukata uhusiano wake wa kidiplomaisa na Ethiopia.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alifanya mkataba na rais wa Somaliland Musa Bihi Abdi January 2023. Picha/Ofisi ya Waziri Mkuu Ethiopia.

"Hakuna nafasi ya upatanishi isipokuwa Ethiopia kubatilisha makubaliano yake haramu na kuthibitisha tena uhuru na uadilifu wa ardhi ya Somalia," serikali ya Somalia imesema katika taarifa.

Somalia imepinga makubaliano hayo ikidai kuwa si halali kwani inachukulia Somaliland kama sehemu ya nchi yake.

"Utawala wa Somalia na uadilifu wa eneo lake umekiukwa na Ethiopia ilipotia saini makubaliano ya kisheria na utawala wa eneo la Kaskazini la Somaliland (nchini Somalia), kinyume chake," taarifa ya Somalia imeongezea.

Ethiopia tayari imefanya makubaliano ya kijeshi na Somaliland.

Nchi hiyo isiyo na bahari na bandari imekataa kuhudhuria mkutano wa mamlaka ya kiserikali ya maendeleo IGAD, ambayo inafanyika Uganda 18 Januari 2024.

Mkutano huo ulipanga kujadili mzozo kati ya Somalia na Ethiopia.

Kupitia taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, nchi hiyo ilidai kuwa haitahudhuria kwani ina shughuli nyengine ambazo zinagongana na ratiba ya mkutano wa marais wa IGAD.

Pia ilidai kuwa wito wa kuhudhuria mkutano huo umekuja ghafla hivyo haukuwapa nafasi ya kutosha kujiandaa.

Djibouti ambayo ni mwenyekiti wa IGAD ilitoa wito kwa wanachama wa IGAD katika mkutano huo tarehe 11 Januari 2023, siku saba kabala ya siku ya mkutano.

kwa sababu hiyo

TRT Afrika