Na Lynne Wachira
TRT Afrika, Nairobi, Kenya
Bingwa wa dunia na Olimpiki Faith Kipyegon wa Kenya alishinda tuzo la mwanariadha bora wa kukimbia Kwenye uwanja baada ya Msimu wa kufana.
Kipyegon aliandikisha rekodi tatu za dunia katika mashindano tofauti na vile vile akatwaa mataji mawili katika mashindano ya dunia ya riadha mjini Budapest.
"Bila shaka ninajivunia msimu wa kipekee, nilifanikiwa kutimiza baadhi ya ndoto zangu" , Kipyegon alielezea furaha yake baada ya kupokea Tuzo lake katika hafla ya shirikisho la Riadha duniani iliyofanyika mjini Monaco.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka ishirini na Tisa Alishiriki mashindano ya ligi ya Diamond mjini Florence nchini Italian na kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500 ya 3:49:11 ikiwa ni ubora wa takriban sekunde moja kutoka kwa rekodi ya zamani.
Licha ya kutokuwa na uzoefu mwingi katika mbio za mita Elfu tano, Kipyegon alijitosa Ulingoni katika mkondo wa Diamond wa mjini Paris Juma moja baadaye. Ni hapa alipowaacha mashabiki Kinywa wazi baada ya kukimbia kwa ueledi wa hali ya juu zaidi huku juhudi zake zikizaa rekodi mpya ya dunia ya 14:05:20 huku akiboresha rekodi ya Awali kwa sekunde 1:42.
Rekodi ya tatu ilikuwa ni katika mbio za maili moja ikiwa ni katika Mashindano ya ligi ya Diamond kwa Mara nyingine tena, wakati huu ikiwa mjini Monaco.
Alishinda mbio hizo kwa muda wa rekodi ya dunia wa 4:07:64 ikiwa ni sekunde tano bora ikilinganishswa na rekodi ya Hapo awali.
Kwa Sasa Kipyegon ataangazia Michezo ya olimpiki huku akilenga historia iwapo atashinda mbio za olimpiki kwa Mara ya tatu mfululizo.
Wanariadha bora wa mwaka katika mashindano ya nje ya Uwanja
Tigist Aseffa na Kevin Kiptum ni wanariadha bora wa mwaka katika mashindano ya nje ya Uwanja
Bila shaka ulikuwa ni mwaka wa kipekee kwa wanaridha wa Afrika huku Kevin Kiptum wa Kenya na Tigist Asseffa wa Ethiopia wakiandikisha rekodi mpya za mbio za marathon.
Mafanikio ya Tigist yalidhihirika wazi wakati wa mashindano ya mbio za marathon za mji mkuu wa Berlin ambapo aliandikisha rekodi ya mpya ya dunia katika mbio za marathon katika muda wa 2:11:53 na Kuboresha rekodi ya zamani ya Bridgid Kosgei kwa dakika mbili na Sekunde 14, hii ikiwa ni Mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 40 rekodi kuboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Ushindi wake ulikuwa wa kipekee Kwani alimaliza takriban dakika sita Kabla ya mwanaridha wa nafasi ya pili kukamilisha mbio.
Katika upande wa wanaume Kevin Kiptum vilevile aliandikisha rekodi mpya ya dunia katika mbio za marathon katika mashindano ya mji mkuu ya Chicago.
Muda wake wa 2:00:35 ni sekunde 34 bora ikilinganishwa na rekodi ya Hapo awali ambayo ilishikiliwa na Mkenya mwingine Eliud Kipchoge.
"Nina furaha isiyo kifani kupokea Tuzo la mwanariadha bora wa mwaka katika mashindano nje ya uwanja, ninawashukuru mashabiki wangu", alisema Kitum kutoka mjini Monaco.
Mafanikio ya Kiptum yanaashiria mwanariadha aliye na uwezo wa kipekee Kwani alibishia Hodi mbio za marathon mwaka uliopita mjini Valencia na vilevile akashinda mbio za mji mkuu wa London mwezi April mwaka huu
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 24 tayari ametajwa katika kikosi cha Kenya cha wanariadha wa marathon wanaotarajiwa kushiriki michezo ya olimpiki mjini Paris.
Wanariadha Chipukizi wa kutazamiwa
Wakenya Faith Cherotich na Emmanuel Wanyonyi walipokea Tuzo za wanaridha chipukizi wa mwaka kupitia mafanikio katika vitengo vyao.
Bingwa hao wawili wa dunia kwa mashindano ya wanariadha wasiozidi mika ishirini walijitosa Kwenye mashindano tofauti katika ulingo wanaridha Wazoefu haswa Kwenye mashindano ya riadha ya dunia mjini Budapest huku Emmanuel Wanyonyi akishinda medali ya fedha katika mbio mia nane huku Faith Cherotich akinyakua Shaba katika mbio za mita elfu tatu kuruka viunzi na maji.
Cherotich, kwa Sasa anaorodheshwa wa pili katika historia ya orodha ya wanaridha bora duniani wasiozidi miaka ishirini baada ya kuandikisha Muda wa kasi wa 8:59:65 aliposhiriki fainali ya ligi ya Diamond mjini Eugene ambapo alimaliza katika nafasi ya tatu.
Kando na fedha ya mashindano ya dunia, Wanyonyi vilevile aliibuka mshindi wa msururu wa ligi ya Diamond msimu wa 2023 baada ya Kunyakua ushindi wakati wa fainali mjini Eugene alipoandikisha Muda wa kasi wa 1:42:80.
Katika hotuba yake, Rais wa shirikisho la riadha duniani Sebastien Coe alisema kuwa ilikuwa ni vingumu kumchagua mwanariadha mmoja kama mwanaridha bora wa mwaka.
"Tumeshuhudia matokeo ya kipekee msimu huu, rekodi nyingi zimevunjwa na wanariadha wengi wamejituma vilivyo katika vitengo mbali mbali, ndiposa tukafanya uamuzi kuwatuza wanariadha 6 katika vitengo tofauti,'' alisema Coe.
Rekodi 23 za dunia zimevunjwa katika vitengo mbali mbali mwaka huu.
Orodha ya wanariadha bora duniani 2023 - Wanawake
- Mwariadha bora wa mwaka kukimbia kwa Uwanja Faith Kipyegon, KEN, 1500m/mile/5000m
- Mwanariadha wa mwaka katika uwanja: Yulimar Rojas, VEN, triple jump
- Wanariadha bora wa mwaka nje ya uwanja: Tigist Assefa, ETH, marathon
Wanariadha bora wa mwaka wa 2023 - Wanaume
- Mwanariadha bora kukimbia kwa uwanja: Noah Lyles, USA, 100m/200m
- Mwanariadha bora katika Uwanja: Mondo Duplantis, SWE, pole vault
- Mwanariadha bora wa mwaka nje ya Uwanja: Kelvin Kiptum, KEN, marathon