Wizara ya Biashara na Ushirikiano nchini Ethiopia imetangaza kanuni mpya kwa wafanyabiashara wanaoingiza nchini unga wa ngano na mafuta ya kula.
Chini ya kanuni hizi, unga wa ngano na mafuta ya kupikia yanayoagizwa kutoka nje ya nchi lazima yaongezewe vitamini kabla ya kuingia nchini na kusambazwa sokoni.
Uamuzi wa kuanzisha viwango hivi vya urutubishaji ulifanywa na Baraza la Viwango mwaka mmoja uliopita, na waagizaji kutoka nje walipewa muda wa mwaka mmoja wa kutolipa ushuru kwa ajili hii.
Hata hivyo, kufikia Julai 2023, muda huu wa kutozwa umekwisha.
Serikali inalalamika kuwa sehemu kubwa ya unga wa ngano ulioagizwa kutoka nje na bidhaa za mafuta ya kula zilishindwa kufikia viwango vya lazima vya urutubishaji vilivyoanzishwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Kulingana na sheria hii mpya, viwanda vya ndani ya nchi vinapaswa kulenga kuimarisha bidhaa katika kiwango cha uzalishaji.
Urutubishaji wa chakula ni nini?
Kulingana na Shirka la Afya Duniani WHO, urutubishaji ni hali ya kuongeza kwa kudhamiria maudhui ya virutubishi vidogo vidogo (yaani, vitamini na madini) katika chakula au kitoweo ili kuboresha lishe ya chakula na kutoa manufaa ya afya ya umma ya afya.
Urutubishaji pia husaidia kuzuia utapiamlo.
"Lishe bora na tofauti zinaweza kutoa vitamini na madini yote yanayohitajika kwa maisha yenye afya. Hata hivyo, kwa watu wengi ni vigumu kupata virutubishi vyote wanavyohitaji kutoka kwa mlo wao pekee," WHO inasema, "Kufikia ulaji uliopendekezwa wa vitamini na madini inaweza kuwa changamoto."
Urutubishaji unaochangia katika kuzuia, kupunguza na kudhibiti upungufu wa virutubishi.
Inaweza kutumika kusahihisha upungufu wa virutubishi katika jamii kwa ujumla au katika vikundi maalum vya watu kama vile watoto, wajawazito na walengwa wa mpango wa ulinzi wa kijamii.
Urutubishaji barani Afrika
Kulingana na Shirika la Kimataifa linalotoa msaada wa kiushauri kwa serikali na mashirika ya kikanda kuhusu urutubishaji wa vyakula-Food Fortification initiative, barani Afrika, nchi 29 zina mamlaka ya kurutubisha unga wa ngano. Nchi kadhaa katika eneo hili huimarisha zaidi ya nusu ya unga wao wa ngano uliosagwa viwandani ingawa si lazima.
Hizi ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Namibia, Sierra Leone na Swaziland.
Inasema kwa kuongezea, nchi nyingi pia huimarisha mafuta ya kupikia, unga wa mahindi, sukari na chumvi kama sehemu ya mkakati wao wa lishe.
Nchini Kenya, mwaka wa 2012 urutubishaji wa unga wa mahindi na ngano na mafuta ya mboga inarutubishwa.
Nchini Tanzania, urutubishaji wa chumvi kwa madini ya iodini ulianza katika miaka ya 1990, na urutubishaji wa unga wa ngano na mahindi na virutubishi vingi na mafuta yenye vitamini A umeidhinishwa na sheria tangu 2011.
Nchini Uganda, urutubishaji wa chumvi kwa iodini ulianza mnamo 1994, na urutubishaji wa unga wa ngano na mahindi na mafuta yenye vitamini A umeidhinishwa na sheria tangu 2012.
Nchini Rwanda serikali ilipitisha sheria mwaka 2018/2019, ya urutubishaji wa chumvi, unga wa ngano, bidhaa ya unga wa mahindi, mafuta ya lkupikia , sukari na chakula cha watoto.