Uchafuzi wa Mazingira  / Photo: AP

"Harakati bado hazijazaa matunda ya kutosha. Nchi nyingi hazitazami jinsi plastiki inavyotumika, mzunguko wa maisha ya plastiki pamoja na inatupwa wapi, inahifadhiwa wapi?" aeleza Ellen Otaru, Mweneyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania, JET.

Angalau nchi 34 za Kiafrika zimechukua hatua kubwa, kupitia marufuku au kodi kubwa, kupunguza uchafu wa plastiki ambao utaishia kwenye mito na bahari zao, ardhi na miili yao. Wananchi wao wanataka hatua zaidi zichukuliwe.

Kulingana na utafiti wa shiriki la kitafiti la Afrobarometer katika nchi 36 mnamo 2021/2022, theluthi mbili (66%) ya Waafrika wanasema uchafuzi ni tatizo kubwa katika jamii zao, ikiwa ni pamoja na 39% ambao wanasema ni "tatizo kubwa sana."

"Ndio maana bahari, mito n.k. bado vinajaa plastiki, viroba na vifungashio ndio nchi zetu zimeweza fanikiwa kutatua kama tatizo ila vifaa vya nyumbani ni stori tofauti." aongeza Otaru.

Zaidi ya watu 77% wanasema mifuko ya plastiki ni chanzo kikubwa cha uchafuzi, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa katika kila nchi iliyofanyiwa utafiti isipokuwa Zimbabwe.

Kwa kushangaza, nane kati ya 10 (79%) wanasema serikali yao inapaswa kuongeza jitihada zake za kupunguza uchafuzi na kulinda mazingira.

"Tusiwe na mtazamo finyu, mifuko ya plastiki imechukuliwa hatua lakini kuna mambo zaidi ya hiyo, kwa mfano taka za viwanda. Sera zinaonyesha kwamba tunapaswa kuacha kutumia plastiki lakini hazijaimarishwa kamwe." Otaru asema.

Kuna haja ya kuwa na njia mbadala au tofauti na plastiki ili watu waache kutumia plastiki asisitiza Ellen Otaru huku akiongeza kuwa watu bado wanatumia plastiki kwa sababu "ni rahisi kutumia na inafanya kazi nzuri zaidi."

Theluthi mbili (66%) - ikiwa ni pamoja na idadi kubwa katika nchi 32 - wanataka kuona hatua "zaidi sana" zikichukuliwa juu ya suala hili. Ni asilimia moja tu ya washiriki (5%) wanadhani serikali inapaswa kufanya kidogo.

Idadi kubwa (ingawa bado ni wachache) wameridhika na jitihada za serikali katika nchi nne: Mauritania (45%), Namibia (35%), Morocco (35%), na Nigeria (24%). Lakini hao ni wachache.

"Moroko na baadhi ya nchi za Kaskazini mwa Afrika zimeainisha na kugawanya plastiki ili kuboresha zaidi njia za kuitoa nje ya matumizi. Tunahitaji kuwekeza katika mipango kama hiyo." Otaru asema.

TRT Afrika