Na Abdulwasiu Hassan
Chokoleti iko katika hali ya kuyeyuka kwani upungufu usio na kifani wa usambazaji kutoka kwa mashamba ya kokoa yaliyopigwa na jua huko Afrika Magharibi unapelekea bei ya zao hilo kupanda maradufu.
Bei ya tani moja ya Kokoa itokayo katika miti ya Theobroma, iliongezeka zaidi ya mara mbili katika miezi michache ya kwanza ya 2024 na kupanda mara tatu had karibu dola za Marekani 10,000, mwaka jana.
Ongezeko la bei limekuwa gumu kwa watengenezaji na watumiaji wa chokoleti, ikidhirika kwa bei ya bidhaa maarufu kama mayai ya Pasaka kwa asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.
Kinyume chake, hii inamaanisha kuwa tani moja ya kokoa sasa ina thamani mara kumi na moja zaidi ya kiwango sawa cha mafuta, na kuwa chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni kwa nchi za Afrika Magharibi kama Nigeria.
Ni kwa vipi misukosuko ya zao hili inayumbisha bara la Afrika?
Kwa pamoja, Ghana, Ivory Coast, Nigeria na Cameroon zinazalisha takribani asilimia 75 ya Kokoa inayopatikana duniani, ikiwa ni dhihirisho kwamba haya lazima yafaidike na ongezeko la bei za malighafi.
Ugumu katika usambazaji
Kwa kuwa sababu kuu ya kupanda kwa bei ya kakao ni kushuka kwa uzalishaji, hii inaweka kikomo moja kwa moja kiwango ambacho wazalishaji wanaweza kufaidika kutokana na ongezeko la bei duniani.
Tafiti mbalimbali zinahusisha kushuka kwa kasi kwa usambazaji wa Kokoa na mambo matatu - uchimbaji haramu wa dhahabu, mabadiliko ya hali ya hewa na kuzeeka, mashamba yaliyojaa magonjwa.
Bodi ya uuzaji ya Kokoa Ghana, Cocobod, inakadiria kuwa hekta 590,000 za mashamba makubwa zimevamiwa magonjwa yanayotishia mazao hayo, kulingana na ripoti ya Reuters.
Mambo haya na mengine yanaleta mtazamo mbaya katika mnyororo wa kimataifa wa usambazaji wa kokoa katika miezi ijayo.
Shirika la Kimataifa la Kokoa linakadiria kuwa usambazaji unatarajiwa kupungua kwa asilimia 11 msimu huu, na kuongeza nakisi ya usambazaji.
Mawazo tofauti
Mgogoro wa kokoa unapozidi kuongezeka, kuna hali ya matarajio miongoni mwa wakulima ambao mashamba yao hadi sasa yameepuka matatizo mbalimbali yanayoathiri sekta nyingine.
Ingawa bado si rasmi, ongezeko lolote la bei na bodi za Kokoa za nchi zinazozalisha zao hilo, gumzo katika soko ni kwamba Ivory Coast tayari imepandisha bei ya lango la shamba kwa 50.
N'koh Ambroise, mtengena chokoleti kutoka Ivory Coast, anafuraha kuhusu kupanda kwa bei ya Kokoa katika soko la kimataifa. "Ni malipo ya haki, kitu ambacho kilipaswa kuja zamani," anaiambia TRT Afrika.
Ambroise hatengenezi tu chokoleti yenye ladha nzuri. Yeye ni mkulima maarufu wa kakao katika nchi yake ya asili. Maharage ya kikaboni kutoka shambani mwake yangegharimu mara tano ya bei ya kokoa ya kawaida hata kabla ya kupanda kwa bei iliyosababishwa na kupungua kwa usambazaji.
Ingawa hii ni tofauti na hisia za watumiaji wa chokoleti na wadau katika biashara ya kusindika Kokoa, Ambroise anaamini kuwa sio sawa kwa bara la Afrika kupata faida finyu katika mnyororo wa thamani. .
"Kwa kiwango hiki, ni dhahiri kuwa ndani ya miaka michache, hakutakuwa na shamba hata moja la kakao. Watoto wa wazalishaji wangependelea kufanya jambo lingine," anaeleza.
Baadhi ya wachambuzi wanaamini kupanda kwa bei ni kuzuri kwa sekta hiyo, ambayo hadi sasa ilileta faida ndogo kwa wakulima, hasa barani Afrika.
Dhana ni kwamba bei ya juu ya Kokoa ingevutia uwekezaji katika mashamba makubwa, ambayo, kwa muda mrefu, yangeziba pengo la usambazaji na kusababisha kupanda kwa bei.