Utendaji wake ulikuwa na utata mkubwa nchini DRC kufuatia kuonekana kutofanya kazi inayoridhisha. Alishutumiwa na mashirika ya kiraia mashariki mwa Kongo kwa kushirikiana na waasi wa M23.
Kupitia maagizo ya Rais wa Kenya, William Ruto, nafasi yake inachukuliwa na Meja Jenerali Alphaxard Muthuri Kiugu. Meja Jenerali Jeff Nyagah, ambaye tayari yuko Nairobi, Kenya, hatakaa bila kazi kwa muda mrefu.
Katika nyadhifa mpya na uteuzi wa maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Kenya, Meja Jenerali Nyagah ameteuliwa kuwa Afisa Mkuu, Kamandi ya Magharibi.
Tangazo hili linakuja saa chache baada ya barua kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Jenerali-Meja Jeff Nyagah anajiuzulu kufuatia usalama wake na vitisho vilivyoanzishwa na serikali ya Kongo kufuatia kutochukua hatua kwa wanajeshi hao nchini DRC.
Akiwasiliana na TRT Afrika, Patrick Muyaya, Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali ya DRC anathibitisha kujiuzulu kwa kamanda wa vikosi vya EACRF nchini Kongo nakuongeza kwamba "barua hii inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii si halisi".