Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Syria kuitembelea Uturuki siku ya Jumatano

Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Syria kuitembelea Uturuki siku ya Jumatano

"Tutaanza na ziara ya Uturuki kesho kama ishara ya kuiwakilisha Syria," alisema Asaad al Shaibani.
Shaibani aliteuliwa kama Waziri wa Mambo ya Nje katika utawaka wa Ahmed al Sharaa baada ya kuondolewa madarakani kwa Assad mwezi Disemba. /Picha: AA

Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad al Shaibani amesema kuwa ataelekea nchini Uturuki siku ya Jumatano katika ziara yake ya kwanza rasmi kwenye nchi inayohifadhi mamilioni ya wakimbizi wa Syria.

"Kama ishara ya kuiwakilisha Syria mpya, tutakuwa na ziara yetu ya kwanza katika jamhuri ya Uturuki," alisema Shaibani siku ya Jumanne kupitia mtandao wake wa X.

Pia aligusia namna Uturuki inavyowaunga mkono Wasyria, ikisema kuwa “haijawahi kuwaacha raia wa Syria ndani ya miaka 14 iliyopita ".

Uturuki ina zaidi ya raia milioni 3 kutoka Syria walioukimbia vita vya kinyama vilivyosababishwa na Bashar al Assad mwaka 2011.

Shaibani aliteuliwa kama Waziri wa Mambo ya Nje katika utawaka wa Ahmed al Sharaa baada ya kuondolewa madarakani kwa Assad mwezi Disemba.

Alihitimu shahada ya uzamili katika Sayansi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Chuo Kikuu Sabahattin Zaim jijini Istanbul.

Ankara imeahidi kuisaidia Syria huku ikiitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia ujenzi mpya wa nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

TRT Afrika