Mnamo Januari 7, 2025 Marekani ilimuwekea vikwazo kiongozi wa kikundi cha Rapid Support Forces Jenarali  Mohamed Hamdan Dagalo, kwa kuhusika na machafuko nchini Sudan./Picha: Wengine

Baadhi ya nchi za Afrika zinakabiliwa na vikwazo vya kimataifa. Kwa mfano, Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea vikwazo Jamhuri ya Kidemokraisa ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ethiopia, Libya, Mali, Zimbabwe, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Darfur kutokana na changamoto za kiusalama.

Kulingana na Marekani na Umoja wa Ulaya, vikwazo hivyo vinalenga kudumisha na kurejesha amani na usalama wa kimataifa kwa mujibu wa kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Mara nyingi, vikwazo ni njia mojawapo ya kuwawekewa zuio viongozi au ndugu za viongozi hao kuingia kwenye nchi fulani au mara nyingine kutoruhusu viongozi hao kuwa na akiba ya mali kwenye nchi zilizotoa vikwazo.

Aina nyingine ya vikwazo huhusisha nchi za Ulaya na Marekani kusitisha mtiririko wa msaada wa kifedha kwa nchi husika pamoja na kusitisha kufanya biashara na nchi hizo, hatua ambayo hupelekea makampuni ya nchi hizo kutokufanya biashara na nchi zilizowekewa vikwazo.

Na pia kuagiza makampuni yao yasifanye biashara na nchi zinazolengwa na vikwazo hivyo.

Athari ya vikwazo vya kimataifa

Vikwazo huwa na athari ikiwa viongozi walioatajwa wana uhusiano wa moja kwa moja na nchi za Marekani na Ulaya. Kwa mfano, wakati wa vita nchini Sudan Kusini vilivyoanza 2013 Marekani iliweka vikwazo kwa baadhi ya viongozi wa serikali na upinzani kutoingia nchini Marekani.

Sudan Kusini iliwekewa vikwazo na Marekani na Umoja wa Ulaya mwaka wa 2014 baada ya vita nchini humo kuzuka mwaka 2013/ Picha: Reuters 

Hata hivyo, hatua hii haikuwa na athari ya moja kwa moja kwani wengi wa viongozi wa Sudan Kusini hawakuwa na biashara yoyote nchini humo.

Aina nyingine ya vikwazo vinaonekana kuwaumiza zaidi wananchi kuliko viongozi wanaolengwa.

Nchini DRC, vikwazo vya kutonunua silaha vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2000, vinalalamikiwa kuwa sababu ya vikosi vya serikali kutokuwa na uwezo wa kutosha wa kujilinda dhidi ya makundi yenye silaha.

Vikwazo vya kifedha navyo vimeathiri kwa kiasi kikubwa uchumi ya nchi kama vile Sudan.

Athari kubwa huwa kwa wananchi wa nchi husika ikiwa vikwazo vinahusisha masuala ya fedha na biashara.

Kwa mfano, hatua ya Marekani kuiondoa Ethiopia katika Mkataba wa Biashara kati ya Mataifa ya Afrika na Marekani (AGOA), kumesababishwa kufungwa kwa viwanda vya nguo nchini Ethiopia.

Hatua hiyo, pia imezifanya Marekani na Ulaya kupunguza fedha za ufadhili kwa nchi hiyo kutokana na vita vya ndani kati ya mwaka 2020 na 2022, ambavyo vilipelekea serikali kukosa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo.

Kuondolewa kwa Ethiopia kutoka kwa mchakato wa AGOA kuliathiri biashara yake wa viwanda/ Picha: AFP 

Vikwazo vya Umoja wa Afrika

"Mchakato mzima wa vikwazo unahitaji kurekebishwa na kuimarishwa," anasema Desire Assogbavi, mtaalamu wa sera na mshauri wa utetezi wa Afrika katika taasisi ya Open Society, katika mahojiano yake na TRT Afrika.

Sheria ya Umoja wa Afrika inaweka wazi kuwa, "Serikali zitakazoingia madarakani kwa njia zisizo za kikatiba hazitaruhusiwa kushiriki katika shughuli za Muungano.”

Kando na kusimamishwa kwa mikutano na shughuli za Umoja wa Afrika, nchi husika pia zinapata vikwazo ya kibiashara na kiuchumi hasa kutoka kwa miungano yao ya kikanda.

Kati ya mwaka 2019 na 2023, Umoja wa Afrika ulizisimamisha nchi sita kujihusisha na masuala ya umoja huo kwa sababu kuwa mabadiliko ya uongozi katika nchu hizo hayakuwa ya kidemokrasia.

Mfano wa nchi hizo ni pamoja na Sudan (Juni 2019 na Oktoba 2021), Mali (Agosti 2020), Guinea (Septemba 2021), Burkina Faso (Januari 2022), Niger (Agosti 2023) na Gabon (Agosti 2023).

Licha ya vikwazo hivyo, bado maadhi ya mataifa barani Afrika yanaendelea na utekelezwaji wa mapinduzi ya kijeshi.

"Ufanisi wa vikwazo vya Umoja wa Afrika mara nyingi unatiliwa shaka kutokana na kuendelea Migogoro na ukiukaji wa haki za binadamu katika bara zima. Suala la msingi liko katika udhaifu utekelezaji,” Nuur Mohamud Sheekh anaiambia TRT Afrika.

Umoja wa Afrika ukiwekea vikwazo nchi lengo mara nyingi huwa ni kuifanya nchi hiyo kurejea katika utaratibu wa kikatiba kupitia uchaguzi hivyo kuruhusu wananchi kutawala

Hata hivyo, historia imeonesha ugumu katika jambo hilo.

"Vikwazo vinapaswa kubaki kama suluhu ya mwisho huku mazungumzo na diplomasia ikipewa kipaumbele kutatua migogoro kwa amani kwa sababu athari za vikwazo ni nzito sana kwa raia wa nchi lengwa,” Sheekh anasema.

Umoja wa Afrika unakosa usawa

"Hakuna uthabiti katika kile ambacho vyombo vya AU vinachukulia kama mabadiliko yasiyo ya kikatiba serikali inayoongoza kwa viwango viwili mara nyingi vinavyoathiriwa na watendaji wa nje. Hii inapunguza mamlaka ya vikwazo,” mtaalam wa Sera za Afrika Assogbavi anaiambia TRT Afrika.

Kwa mfano nchini Chad, ikiwa chini ya utawala wa Rais wa wakati wa huo Idriss Deby aliuawa 2021, mtoto wake Mahamat Deby, afisa wa kijeshi alichukua uongozi.

Kama ilivyo kawaida ya Umoja wa Afrika ilitarajiwa kuwa Chad ingesimamishwa kwa shughuli za AU baada ya Deby kushindwa kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Hata hivyo Chad haikusimamishwa na AU kwa muda. Deby pia alienda kinyume na ahadi aliyoitoa kwa AU na kugombea Urais na katika uchaguzi wa Mei 6, 2024 alishinda kiti cha Urais.

Vikwazo vya AU vinahitaji marekebisho

"AU inapaswa kufafanua kwa uwazi dhana na taswira ya mfumo wa vikwazo unaoendelea zaidi ya kusimamishwa kwa nchi kutoka kwa shirika,” Assogbavi anasema.

Uungwaji mkono kutoka kwa wakazi wa mitaa kwa viongozi wa kijeshi ambao wanawaona kama "wakombozi" kutokana na kile walichohisi kuwa watawala wasiofaa walioingia madarakani kwa kura, unaongeza katika kudhoofisha utawala wa vikwazo vya AU.

Mali, Burkina Faso na Niger ambazo bado zimewekewa vikwazo na Umoja wa Afrika, hazijapata walizingatia uhamishaji wa madaraka kwa utawala wa kiraia kupitia uchaguzi na hata wameamua kufanya hivyo hawataki kuwa sehemu ya kanda ya Afrika Magharibi ya Umoja wa Afrika, ECOWAS.

"Uwazi na uwajibikaji unapaswa kuimarishwa kwa kuchapisha miongozo iliyo wazi ya utekelezaji wa vikwazo na kuripoti mara kwa mara athari zake,” anapendekeza Nuur ambaye anasema AU lazima ianzishe chombo maalum cha utekelezaji chenye mamlaka ya kufuatilia uzingatiaji na kutoa adhabu kwa ukiukaji.

TRT Afrika