Serikali ya Uganda inasema rais Yoweri Museveni yupo katika afya mzuri

Serikali ya Uganda imetoa taarifa ya uhakika kuhusu hali ya afya ya rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa akipambani na UVIKO-19 tangu tarehe 7 Juni.

"Jenerali... anapata nafuu haraka kutoka kwa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Uviko yaani," taarifa kwenye mitandao ya kijamii umesema.

Kumekuwa na uvumi katika mitandao kuhusu hali ya afya ya rais Museveni ikiwa watu wengine wakidai kuwa amezidiwa na ugonjwa na wengine kudai ameaga dunia.

Katibu Mkuu wa ofisi ya Rais Dkt. Kenneth Omona amesema "yuko katika hali nzuri na anaendelea kupata nafuu."

Tangu kuambukizwa na virusi wa Uviko-19 tarehe 7 Juni, Rais Museveni amekuwa akiandika barua kwa wananchi wake kupitia mtandao wa kijamii.

Lakini hakuandika tarehe 12 Juni , na hapo kupelekea watu kueneza uvumi zaidi kuwa huenda mambo si mazuri kwa afya yake .

Katika ukurasa zake mtandaoni Museveni amekuwa akiwashauri wananchi wake kupata chanjo kamili dhidi ya UVIKO-19 na wazee wapate chanjo nyongeza.

Baadhi ya wananchi nchni Uganda wamekuwa wakimtumia maombi ya kupona kwa haraka, na wengine wamefanya mikutano ya maombi katika maeneo yake wakiomwombea afya njema.

Raia pia wanaruhusiwa kutoa ujumbe wowote kwenye lango la Ikulu.

Majukumu yake ya uongozi amemuachia waziri mkuu wa nchi.

TRT Afrika