Mamlaka ya Udhibiti wa Manufaa ya Umma nchini Kenya imesema inafanya utafiti kuhusu mashirika yasiyo ya serikali yaliyotajwa na serikali kwa uchochezi wa maandamano / Picha: PBO Kenya 

Mamlaka ya Udhibiti wa Manufaa ya Umma nchini Kenya yaani The Public Benefit Regulatory Authority, PBO imesema inafanya utafiti kuhusu mashirika yaliyoshutumiwa kupokea fedha za usajili za kigeni.

Imesema inafanya utafiti kuhusu mashirika yaliyovunja sheria baada ya Rais William kuilaumu shirika la Marekani Ford Foundation kuchochea maandamano ambayo yamepinga uongozi wake tangu Juni 2024.

Wizara ya mambo ya nje iliitaka Ford Foundation kuelezea kwa nini iliizipa mashirika 16 ruzuku ya thamani ya dola milioni $5.78.

" Kati ya mashirika 16 yaliyoorodheshwa katika mawasiliano na Idara ya Masuala ya Kigeni ni matatu tu ndio yamesajiliwa chini ya Sheria ya PBOs ya 2013 ambapo mengine yote yamesajiliwa na Msajili wa Vyama na Makampuni," Mwambu Mabongah mwenyekiti wa PBO amesema.

Hizo ni pamoja na SHOFCO, Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu, KNHCR na Shirika laTransform Empowerment for Action Initiative.

"Mamlaka imetuma kwa Kitengo cha makosa ya jina, DCI kwa uchunguzi zaidi, Mashirika ya Umma ambayo kwa sasa yanafanya kazi bila ya kupata usajili unaohitajika na bado PBOs zinazohusika zinapokea fedha ambazo haziwajibiki kuendesha akaunti za benki ambazo hazijaidhinishwa na kutekeleza miradi ambayo haiwezi kuhesabiwa," Mabongah amesema.

Shirika la Marekani la Ford Foundation liliandikia serikali ya Kenya na kujitoa katika lawama yoyote ya kuchochea maandamano nchini Kenya.

"Utoaji ruzuku wetu ni wa wazi na unapatikana kwa urahisi kwenye tovuti yetu. Hii inajumuisha hifadhi data inayoonyesha pesa zetu zinakwenda wapi," taarifa yake illisema.

TRT Afrika