Safari ya kutoroka vita Sudan, simulizi ya kweli ya raia wa Tanzania na Kenya

Safari ya kutoroka vita Sudan, simulizi ya kweli ya raia wa Tanzania na Kenya

Je, maisha yakoje kwa watu wa Afrika Mashariki wanaorejea nyumbani kutoka Sudan na wanahitaji msaada gani?
 / Photo: Reuters

Maelfu ya watu kutoka duniani kote wanajaribu kurudi nyumbani kutoka nchi ya Afrika Kaskazini ya Sudan, ambako ghasia zimesababisha mamia ya vifo.

Kutokana na mapigano kati ya jeshi la Sudan na Rapid Support Forces, RSF, wengi wamekuwa wakielekea katika nchi za mpakani za Ethiopia na Sudan Kusini kwa usaidizi kutoka kwa balozi zao, ambapo wanaelekea katika nchi zao kupitia njia zinazofikika zaidi.

Wananchi wa Afrika Mashariki wametumia njia zinazoelekea katika mji wa mpakani wa Ethiopia na Sudan wa Gallabat na Metema.

"Siku tano zilizopita, nilijumuika na wananchi wenzangu kutoka Kenya katika eneo maalumu la Khartoum linaloitwa, Araak City, sehemu maalumu ya Wakenya kukutana kama ilivyoelekezwa na Ubalozi wa Kenya nchini Sudan", anaeleza Hamis Ngare kwa TRT Afrika.

Ngare alikata tamaa ya kusubiri taarifa kutoka kwa ubalozi huo alipoona kuwa siku mbili za taarifa zisizojitosheleza zinazidisha hali ya hatari katika eneo hilo. "Balozi hakupatikana na nyumba zilizotolewa huko Araak zilikuwa zimejaa kupita kiasi."

Alielekea katika mji wa mpakani wa Gallabat, ulio kilomita 568 kusini mashariki kutoka Khartoum.

"Tulikuwa katika safari ya basi ya masaa 16 jana, kutoka Khartoum hadi al Qadarif, ambapo ilibidi kubadilisha mabasi kuanza safari nyingine ya masaa 5 hadi mpaka wa Metema," aliongeza.

Kuondoka kwake Sudan ni changamoto kwani amekuwa akifanya kazi Khartoum kama mwalimu kwa miaka kumi, na mtoto wake wa kike, ambaye ni mtoto wa pili, alijifungua siku nane baada ya mzozo kuanza.

Kuna kivuko cha mpakani chenye shughuli nyingi, ambapo watu wamesafiri kutafuta hifadhi na uokoaji nchini Ethiopia. Jana usiku watu walilala kwenye mabasi katika mji wa mpakani ambapo baadhi ya watu walionekana wakiwa na chochote walichoweza kubeba kutoka Khartoum ili watoke nje ya nchi haraka.

“Safari ilikuwa hatari sana kwetu mpaka mpakani; tulipokuwa tukivuka mpaka, tulisikia mashambulio ya anga kwa mbali. "aliongeza Ngare, ambaye alilazimika kutafuta njia ya kufika mpakani kupitia usafiri wa kibinafsi.

"Serikali ilitoa basi moja ya kuelekea mpakani siku ya Jumatatu na Ubalozi haujaturudia tena kwetu ni lini basi linalofuata litaondoka Khartoum."

Yusuf Muleri Faraj, Mhasibu jijini Khartoum kwa miaka minane, ni Mkenya kutoka Nairobi ambaye anaiambia TRT Afrika kwamba kwake sauti ya bunduki na mabomu si jambo geni na haitoshi kumfanya aondoke mjini.

"ni jambo la kawaida" kwake kwani tangu kipindi cha maandamano ya 2019, nchini Sudan, milio ya risasi na milipuko ilikuwa ni jambo la kawaida. Lakini mnamo Aprili 15, "njia ambayo risasi zilikuwa zikifyetuliwa ilikuwa tofauti kidogo."

“Siogopi. Mke wangu aliogopa sana na tuna mtoto wa miezi tisa hivyo. Kama mwanaume sihitaji kuwa na wasiwasi au hata kuonyesha woga na kuwa mwanaume katika haya yote, ninahitaji kufanya maamuzi sahihi.” Faraj anaeleza.

Ikiwa serikali haitakuwa mpakani, Faraj ataelekea Gondar na kulala huko kwa usiku huo, kwa kuwa mtoto wake mchanga wa miezi minane atazingatiwa. Mara tu atakapotoka Gondar, na ikiwa fedha zake zitamruhusu, ataelekea Uwanja wa Ndege nchini Ethiopia kupanda ndege ya kurejea nyumbani.

Bado haijafahamika ni saa ngapi, au ni lini serikali ya Kenya itafika mpakani huku Wakenya kadhaa wakihofia rasilimali kama vile pesa na chakula kuisha.

Haikuwa safari mbaya kwa kila mtu

Kulikuwa na utaratibu mzuri kwa Watanzania walioondoka Khartoum. Ndege ya kwanza kutoka Tanzania iliyoondoka Ethiopia ikiwa na abiria kutoka Sudan imetua leo asubuhi.

Humaida Mussa Yusuph ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika mjini Khartoum, alieleza kuwa kilichokuwa kikiendelea nchini Sudan kiligeuka kuwa suala la kuchukuliwa kwa uzito wakati zaidi ya siku mbili za milio ya risasi sasa ilionekana kutokuwa ya kawaida. Kuongeza kuwa "... jumuiya ya kimataifa kuhutubia ilikuwa ushahidi kwamba kuna kitu kibaya kinaendelea."

"Katika kundi letu la Whatsapp la Chuo Kikuu tuliarifiwa kwamba tujiandae kuondoka na basi kwa ajili ya Watanzania wanaokwenda Ethiopia na taarifa hizo zilitoka ubalozini."

Watanzania kutoka Khartoum walondoka katika msafara wa mabasi yaliyofanya safari ya siku mbili kuelekea Gondar Kaskazini mwa Ethiopia.

“Hakuna Mtanzania aliyeachwa nyuma, tulipofika mpakani kila kitu kilishughulikiwa na ubalozi, hatukusubiri hata muda mrefu. Muda wa kutayarisha vibali na makaratasi ya kuvuka mpaka haikuwa ndefu hivyo.

Kutoka Gondar, Watanzania hao walipanda ndege ndogo hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa. "Tulipanda ndege hizi ndogo kuelekea Addiss Ababa na tukakuta Air Tanzania ilikuwa inatusubiri."

Ndege ya shirika la ndege la Air Tanzania aina ya Boeing Dreamliner ilitumwa kuwasafirisha wakazi wa Tanzania kutoka Bole hadi Dar es Salaam, nchini Tanzania, ambako waliwasili saa 9 asubuhi ya leo. "Nilifika uwanja wa ndege na tulipata mapokezi kutoka kwa maafisa wa serikali, idadi kubwa ya vyombo vya habari na bila shaka familia yangu." anaeleza Bi Yusuph.

"Naipongeza sana kazi iliyofanywa na balozi (Silima Kombo Haji) ambaye tulikuwa naye, tangu tulipotoka Khartoum hadi kutua Dar es Salaam." Yusuph alihitimisha.

Mzozo nchini Sudan uko katika siku yake ya 12 na unasababisha wenyeji kuondoka nchini humo pia katika juhudi za kutafuta faraja mbali na majenerali wanaopigana.

TRT Afrika