Katika amri ya utendaji iliyotiwa saini mwezi huu wa Aprili ambayo sasa impowazi kwa vyombo vya habari, rais wa Uganda Yoweri Museveni anonyesha wasiwasi wake kuhusu utupaji duni wa takataka.
"Ninapoendesha gari kuzunguka Kampala na katika baadhi ya maeneo ya mashambani naona marundo ya takataka vimetawanyika katika maeneo ya wazi. Hii isionekane tena ndani ya miezi sita, lazima ikome." rais amesema katika agizo hili.
Rais anasema Uganda miji lazima iwe safi na ya kukaribisha.
Joseph Masembe mtaalamu wa uhifadhi wa mazingira anasema hii ni hatua nzuri ya kusafisha miji .
Je , agizo hili la rais linataka nini?
- Uwepo wa pipa la takataka kwa kila mita 200 katika kila mji
- Takataka katika pipa hizi zinapaswa kutolewa ndani ya siku tatu au hata kabla ya hii.
- Kuwe na mpango wa kuchakata taka zilizo kusanywa
- Takataka ya plastiki ichakatwe kuwa vitu vinavyoweza kutumika tena kama mifuko
- Takataka za mabaki ya chakula zichakatwe kuwa mbolea aina ya mboji
- Agizo linauliza maoni ya ubunifu kuhusu nini kinapaswa kufanyika kudhibiti takataka za glasi na taka za nguo
Kauli ya Museveni inakuja katika kipindi ambacho mvua zinanyesha katika baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki ambapo viongozi katika maeneo husika wamekuwa wakisisitiza usafi wa mazingira ili kuepukana na maradhi ya milipuko