Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi siku ya Jumamosi alionya dhidi ya upanuzi wowote wa mzozo huko Gaza, akisema eneo hilo linaweza kuwa "bomu la kulipuka wakato wowote".
Pia alisema mamlaka ya nchi yake inapaswa kuheshimiwa baada ya ndege zisizo na rubani kunaswa baada ya kuingia anga ya Misri siku ya Ijumaa.
Israel siku ya Ijumaa ilisema kuwa ndiyo shabaha ya ndege zisizo na rubani ambazo ililaumu vuguvugu la Houthi la Yemen linaloungwa mkono na Iran. Jeshi la Misri limesema ndege hizo zisizo na rubani, zilizoanguka katika miji ya Taba na Nuweiba ya Misri karibu na mpaka wa Israel, na kujeruhi watu sita, zilianzia kusini mwa Bahari Nyekundu. Haijasema ni nani aliyerusha ndege hizo zisizo na rubani.
"Bila kujali inatoka wapi, nimeonya kuhusu kupanuka kwa mzozo huo. Eneo hili litakuwa bomu la wakati ambalo linatuathiri sisi sote," Sisi alisema, akizungumza katika mkutano.
Kumekuwa na wasiwasi kutoka nchi jirani kuwa vita vinavyoendelea ndani ya Gaza vinatishia kusambaa nje ya Palestina huku hisia za hamaki zikipanda kutoka kwa wnaaounga mkono Palestina.
Jordan na Lebanon pia wameelezea wasiwasi wao kuwa huenda vita hivi viukavuka mipaka yao.
Hii ilisababisha nchi hizo kukataa kuwapokea wakimbizi wa Palestina walipokuwa wanafurushwa
Misri imekuwa katika mstari wa mbele kujaribu kutatua mzozo wa Palestina ikiwemo kuandaa kikao cha viongozi wa dunia mjini Cairo, na kufungua mpaka wake wa Rafah ili kuruhusu misaada kupitishwa.