Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema kuwa haiwezekani kuwahamisha wagonjwa bila kuhatarisha maisha yao Gaza.
"Hospitali zote Gaza tayari zinafanya kazi zaidi kutokana na majeraha yaliyopatikana katika wiki za mashambulizi ya mara kwa mara, na haziwezi kustahimili ongezeko kubwa la idadi ya wagonjwa, huku wakihifadhi maelfu ya raia," taarifa kutoka WHO imesema.
Wafanyakazi wa afya, wagonjwa na raia wamekabiliwa na changamoto ya kukosa kwa uwezo wa mawasiliano na kukatika kwa umeme.
"Raia, wagonjwa na wafanyakazi wa afya huko Gaza wamelala usiku kucha katika giza na hofu," anasema Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom.
"Kila saa kuna watu wanaojeruhiwa, lakini gari za wagonjwa haziwezi kuwafikia kutokana na kukatwa kwa mawasiliano huku vyumba vya kuhifadhi maiti vikiwa vimejaa.
Zaidi ya nusu ya waliofariki ni wanawake na watoto," WHO imesema.
WHO inasema pia haijaweza kuwasiliana na wafanyikazi wake huko Gaza, na wa mashirika mengine.