Waandamanaji wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kupinga ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Waislamu mjini Melbourne, nchini Austria, Machi 19, 2019./Picha: Getty

Austria imekuwa na idadi kubwa ya matukio ya chuki dhidi wa Uislamu kwa mwaka jana toka ilipoanza kuorodhesha matukio ya aina hiyo mwaka 2015, kulingana na ripoti iliyotolewa siku ya Jumatatu.

Ripoti hiyo ilichapishwa kwenye tovuti ya kituo kinachoshughulikia chuki na ubaguzi wa rangi dhidi ya uislamu.

Kulingana na ripori hiyo, matukio hayo yameongezeka marudufu toka kuanza kwa vita kati ya Israeli na Hamas, Oktoba 7 mwaka jana.

Matukio zaidi yaliripotiwa kati ya mwezi Oktoba hadi Disemba kuliko miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2023.

Ripoti hiyo ilisema kuwa matukio hayo yalifanyika zaidi kwenye sekta ya elimu, kama ilivyoripotiwa na wazazi, walimu na wanafunzi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, asilimia 66.7 ya matukio hayo yalifanyika mitandaoni wakati asilimia 33.7 kwa njia ya kawaida.

Asilimia 87.8 ya matukio yaliyorekodiwa mitandaoni ilihusu kuenea kwa chuki.

Kulingana na ripoti hiyo, Waislamu walidhihakiwa kama wanyama kupitia machapisho ya mitandaoni.

Ripoti hiyo ilisema kuwa asilimia 40.8 ya matukio yoyote ilihusisha manyanyaso wakati asilimia 19.5 ilihusisha matusi. Kusambaa kwa chuki kulichangia asilimia 8.9 wakati asilimia 2.6 ilihusisha mashambulizi ya kimwili.

Kulingana na ripoti hiyo, matukio mengine yalihusisha uharibifu(asilimia 7.5), manyanyaso ya polisi (asilimia 7.3), vitisho vya hatari (3.2), uchochezi wa chuki(1.8), dhihaka (0.8) na mengineyo (7.7)

Katika ripoti yake, kituo hicho kilisisitiza kwamba takwimu zake ni muhtasari na kwamba idadi halisi ya kesi inadhaniwa kuwa kubwa zaidi.

Shirika linaona takwimu hizi kama "maendeleo ya wasiwasi" ambayo yanazidi kuchangia mgawanyiko katika jamii.

Kituo hicho kilitoa wito wa kushughulikia masula hayo.

TRT Afrika
AA