Rais wa Cameroon Paul biya amefanya mageuzi katika uongozi wa wizara ya ulinzi  / Picha: Reuters

Rais wa Cameroon Paul Biya amefanya uteuzi mpya katika wizara ya ulinzi.

Mabadiliko yaliyoandikwa katika taarifa na rais Biya yanaathiri utawala wa kijeshi wa nchi hiyo.

Mabadiliko haya yamekuja siku moja baada ya majeshi katika nchi jirani ya Gabon kunyakua mamlaka na kumweka rais Ali Bongo Ondimba kizuizini nyumbani.

Hii ni mara ya tatu anafanya mabadiliko ya kijeshi mwaka huu Cameroon.

Wanajeshi Gabon wamejaribu kupindua serikali baada ya rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 26 Agosti.

Viongozi wa mapinduzi ya Gabon wamemteua Jenerali Brice Oligui Nguema kuwa kiongozi mpya wa nchi hiyo.

Rais Biya wa Cameroon mwenye umri ya miaka 90 , anahudumu kwa muhula wa saba madarakani baada ya kuingia mamlakani mwaka wa 1982.

Kufikia sasa rais Biya amekuwa rais wa Cameroon kwa miaka 40.

Uchaguzi wa urais Cameroon mwaka 2018 ulikumbwa na idadi ndogo ya waliojitokeza kupiga kura na madai ya vitisho vya kura.

Rais asiyekuwepo

Rais Paul Biya amekashifiwa kwa kuwa rais anayeongoza Cameroon kutoka ulaya.

Rais Paul Biya na mkewe Chantal Biya wanakashifiwa kwa kutumia rasilimali mingi kuzuru ulaya  / Picha: AFP 

Kwa mfano mnamo 2006 na 2009, Biya alitumia theluthi moja ya mwaka nje ya nchi.

Mwaka 2018 alitumia siku 60 kwa ziara nje ya nchi.

Mwezi Juni mwaka huu , rais Biya alisafiri kwenda Paris, Ufaransa kwa mkutano wa marais wa mabadiliko ya tabianchi, lakini hata baada ya mkutano hakuonekana nchini kwa zaidi ya mwezi mmoja badae.

Maisha yake hasa katika nchi ya Switzerland, ikiwa anasemekana kupenda hoteli ya Intercontinenetal, jijini Geneva, imezua mjadala mkali kwa muda mrefu miongoni mwa Wacameroon.

TRT Afrika