Rais Denis Sassou-Nguesso ana umri ya miaka 79  / Picha: AFP

Kumeibuka hali ya wasiwasi nchini Congo Brazaville baada ya taarifa ya jaribio la mapinduzi kuenea katika mitandao ya kijamii nchini humo.

Hata hivyo, jeshi la nchi hiyo limekanusha taarifa hiyo mara moja. Hayo yanajiri, wakati ambapo rais Denis Sassou-Nguesso yuko nchi Marekani akihudhuria mkutano wa marais wa Umoja wa Mataifa.

Lakini baada tu ya kuibuka kwa taarifa hizo, watu wamekuwa na shauku ya kutaka kumjua zaidi rais Denis Sassou-Nguesso mwenye umri ya miaka 79.

Denis Sassou-Nguesso ni nani?

Rais Denis Sassou-Nguesso ni mwanasiasa na kiongozi wa zamani wa kijeshi ambapo alipata mafunzo yake ya kijeshi nchini Algeria na Ufaransa.

Sassou Nguesso aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi mwaka 1975 / Picha: Others 

Congo inapakana na Angola , Gabon, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo nma Jamhuri ya Afrika ya kati.

Mwaka 1963 Sassou-Nguesso aliteuliwa kuwa kamanda wa vikosi vya jeshi huko Brazzaville na mwanzoni mwa miaka ya 1970 alipanda cheo cha kanali. Alihusika katika mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1968 ambayo yaliyomuondoa madarakani rais Massemba Debat na kumuweka madarakani Marien Ngouabi.

Sassou Nguesso aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi mwaka 1975 akiwa na umri wa miaka 32 tu tarehe 18 Machi 1977, pindi alipouawa rais Marien Ngouabi. Jeshi lilichukua udhibiti wa serikali na Sassou-Nguesso aliteuliwa kuwa rais mnamo Februari 8, 1979.

Kuanza safari ya urais

Tarehe 8 Julai, 1979 uchaguzi ulifanyika na Sassou-Nguesso alichaguliwa kuwa rais. alichaguliwa tena mnamo 1984 na 1989. Katika uchaguzi wa mwaka 1992, Sassou-Nguesso aliondolewa katika duru ya kwanza.

Mnamo 2021 Sassou-Nguesso alichaguliwa kwa muhula mwingine wa miaka mitano/ Picha: Others 

Mwanasiasa mwingine, Pascal Lassouba alichaguliwa kuwa rais. Lakini mwaka 1993 mapigano yalizuka kati ya wanaomuunga mkono Lassouba na Sassou-Nguesso.

Vita ambavyo viliendela mpaka 1999 ambapo maelfu walipoteza maisha na zaidi ya laki 8 walikimbia makazi yao.

Sassou-Nguesso alichaguliwa tena mwaka 2009 na mwaka 2015 katiba ya nchi hiyo ilibadilishwa ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu.

Katika uchaguzi wa Machi 2016, alichaguliwa tena lakini waangalizi wengi waliamini mchakato wa uchaguzi huo haukuwa wa haki.

Mnamo 2021 Sassou-Nguesso alichaguliwa kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Taarifa hizi zinatokea wakati ambapo tayari kumekuwa na wimbi la mapinduzi katika nchi mbalimbali ikiwemo Niger, Gabon na Mali.

TRT Afrika