Kenya ni kati ya nchi zilizotuma wanajeshi nchini DRC chini ya Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki,  Mashariki mwa DRC/  Picha kutoka EACCRF

Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mashariki mwa DRC imesema 'mapigano mabaya yalimjeruhi vibaya askari wa kulinda amani wa Kenya' mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

"Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na M23 yalivunjwa," kikosi hicho kimesema katika taarifa.

"Mapigano hayo mabaya yalimjeruhi vibaya askari wa kulinda amani wa Kenya aliyekuwa Kanyamahoro karibu na Kibumba, kilomita 15 Kaskazini Mashariki mwa Goma," imeongezea kusema taarifa hiyo.

Kikosi cha jeshi cha kikanda kilitumwa kwa mara ya kwanza mashariki mwa DRC mwezi Novemba 2022.

Tangu wakati huo, kimekuwa na jukumu muhimu katika kuwezesha mafanikio ya usitishaji mapigano katika maeneo mengi ambapo Vikosi vya Wanajeshi wa Kongo (FARDC) na kundi la waasi wa M23 walikuwa wakipigana.

Kikosi hicho kinasema uchunguzi utafanywa ili kubaini mwanajeshi huyo ameuawa katika mazingira gani.

Hata hivyo, bado jeshi la Taifa la Kenya halijatoa maelezo rasmi kuhusu mwanajeshi huyo ambaye aliuawa akiwa kazini.

Hali ya mashariki mwa DRC imekuwa jambo la kutia wasiwasi Jumuiya ya Kimataifa kutokana na ghasia za muda mrefu na athari zake kwa raia.

TRT Afrika