Viongozi wa kijeshi wa Gabon, ambao walimpindua Rais Ali Bongo Ondimba mwezi Agosti, wametangaza kwamba uchaguzi utafanyika mwezi Agosti 2025 kulingana na ratiba ambayo kwanza itaanza na mazungumzo ya kitaifa.
"Agosti 2025: uchaguzi na mwisho wa mpito," msemaji wa utawala alisema kwenye televisheni ya taifa siku ya Jumatatu.
Muda huo utawasilishwa kwenye mkutano wa kitaifa utakaoundwa na "wadau muhimu" wote wa nchi, uliopangwa kufanyika mwezi Aprili 2024.
Utawala wa mpito pia ulitangaza kwamba rasimu ya katiba itawasilishwa mwishoni mwa mwezi Oktoba 2024, na kura ya maoni juu ya kupitishwa kwake itafanyika takribani Novemba-Desemba 2024.
TRT Afrika na mashirika ya habari