Patrick Herminie | Picha: AP

Patrick Herminie, kiongozi wa chama cha United Seychelles na mgombea katika uchaguzi wa urais wa 2025, alilaani uamuzi huo kama wa kisiasa.

Bwana Herminie alikamatwa Ijumaa katika makao makuu ya chama chake ambayo pia ni ofisi yake kabla ya kuachiliwa.

Patrick Herminie, pamoja na watu wengine sita wa Ushelisheli na raia wa Tanzania, wameshtakiwa kuhusiana na uchunguzi wa "ushirikina" na "vitendo visivyo vya kawaida na vya kishirikina."

Uchunguzi huo unaohusiana na ugunduzi mwezi Agosti wa maiti za mwanamke na kijana mdogo katika makaburi kisiwani Mahé.

Jina la Bwana Herminie, ambaye alikuwa rais wa Bunge la Taifa kati ya 2007 na 2016, lilipatikana kwenye simu ya raia wa Tanzania, ambaye alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shelisheli mwishoni mwa Septemba akiwa na mawe, chupa ndogo zenye vimiminiko vya rangi ya kahawa, unga ndani ya chupa nyingine, na hati kadhaa zilizo na lugha na alama zisizoeleweka, hayo ni kulingana na Shirika la Habari la Shelisheli.

Mwendesha mashtaka walisema kuwa alama kwenye hati hizo zilikuwa sawa na nyengine zilizopatikana katika maeneo yaliyoharibiwa katika visiwa hiyvo.

Baada ya kushtakiwa Jumatatu, Patrick Herminie aliachiliwa kwa dhamana ya rupe ya Shelisheli 30,000 (karibu $2,200).

"Kwa maoni yangu, huu ni uamuzi unaoletwa moja kwa moja kutoka kwa urais wa Bwana Ramkalawan, " Bwana Herminie, aliiambia vyombo vya habari Ijumaa.

Ikiwa watakutwa na hatia, washukiwa wanaweza kutozwa faini. Kesi itaendelea kusikilizwa tarehe 3 Novemba.

TRT Afrika