RAis Willim Ruto amewafuta kazi makatibu wa baraza au nawaziri wake 22/ Picha Ikulu Kenya 

Rais William Ruto wa Kenya ametengua baraza lake la mawaziri.

"Nimeamua mara moja kuwafuta kazi makatibu wote wa Baraza la Mawaziri na Mwanasheria Mkuu, isipokuwa katibu mkuu na mawaziri wa Mambo ya Nje na bila shaka Ofisi ya Naibu Rais haiathiriwi kwa vyovyote vile," Rais William Ruto amesema katika taarifa kwa nchi aliyotoa Ijumaa katika Ikulu, Nairobi.

Rais Ruto amesema maamuzi yake yametokana na kuwasilkiliza Wakenya na kuangalia kazi za mawaziri wake.

"Nitashiriki moja kwa moja katika mashauriano ya kina katika sekta mbalimbali na miundo ya kisiasa na Wakenya wengine hadharani na kibinafsi kwa lengo la kuunda serikali pana ambayo itanisaidia katika kuharakisha utekelezaji muhimu na wa haraka usioweza kuyumbishwa," Rais Ruto amesema.

"Tumejumuisha hatua na mipango mengine mikali ya kushughulikia mzigo wa deni ili kuchunguza kuongeza rasilimali na mapato ya ndani, kupanua nafasi za kazi, kuondoa upotevu wa rasilimali, kuua joka la ufisadi, na hivyo kuifanya serikali ya Kenya kuwa na gharama nafuu na ufanisi," Rais Ruto aliongezea.

Vijana Gen Z walifanya maandamano kwa wiki tatu, kwanza wakipinga muswada wa fedha 2023. Baada ya Rais Ruto kukubali kuutupilia mbali muswada huo, waandamanaji waliendelea wakipinga uongozi wake na hata kumtaka ajiuzulu.

Julai 9, 2024 Rais Ruto alitia saini muswada wa kuunda upya Tume ya uchaguzi, IEBC.

TRT Afrika