Tangazo hilo la televisheni linamuonyesha afisa wa trafiki akipewa kinywaji na baadae anamuachilia dereva mwenye makosa / Picha Polisi Uganda.

Uongozi wa polisi nchini Uganda umelaani vikali utumiaji wa sare ya vikosi vya usalama barabarani yani trafiki, katika tangazo la biashara lenye utata, la kinywaji, maarufu kwa jina la "JESA JUS."

Tangazo hilo la televisheni linamuonyesha polisi trafiki, wakati wa kutekeleza majukumu yake, akimsimamisha dereva kwa ajili ya ukaguzi.

Lakini dereva akampa pakiti ya kinywaji cha JESA JUS, na hapo akamwachia aendelee na safari yake bila ukaguzi.

Askari huyo ameonekana akisema, "Unaweza kwenda", baada ya kuchukua "JESA JUS."

"Tangazo linaashiria kuwa polisi ni wafisadi na wanapokea hongo kwa urahisi na "JESA JUS," polisi imesema katika taarifa yake.

"Dereva huyo anaonekana akidaiwa kumhonga askari akiwa na pakiti ya JESA JUS mbele ya watoto na hatimae kuwaanchia," imeongezea.

Polisi ya Uganda inasema tangazo hilo linaimarisha mtazamo hasi wa watoto dhidi ya polisi.

TRT Afrika