Chama cha CHADEMA nchini Tanzania kilitoa  tangazo hili kwa mitandao kikitaka polisi kuachilia viongoiz wake photo by CHADEMA/ Picha: CHADEMA 

Wanasiasa maarufu wa Tanzania Freeman Mbowe na Tundu Lissu walikuwa miongoni mwa maafisa wa upinzani walioachiliwa kutoka kizuizini na polisi Jumatatu usiku kufuatia kukamatwa kwao, polisi walisema.

"Wamesafirishwa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi mpaka majumbani kwao kutokea maeneo mbalimbali waliokuwa wanashikiliwa yaani Njombe , Songwe, Iringa na Mbeya," ameelezea John Mrema, msemaji wa CHADEMA.

Mamia ya wafuasi wa vijana ambao pia walikamatwa siku ya Jumapili katika mji wa kusini-magharibi mwa Mbeya, katika mkesha wa mkutano wao uliopangwa kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani, waliachiliwa baada ya kuhojiwa.

Afisa wa polisi Awadhi Haji aliviambia vyombo vya habari vya ndani.

"Viongozi wakuu wamesafirishwa usiku kwa njia ya barabara na wamepokelewa kituo cha Polisi kati Dar es Salaam, watatakiwa kujidhamini, kisha kupelekwa majumbani asubuhi ya leo tarehe, 13.08.24," CHADEMA imesema katika mtandao wake wa X.

"Ofisi za chama Mbeya zimezingirwa na Polisi na hawaruhusu watu kuingia katika ofisi hizo," imeongezea.

Polisi wa Tanzania walikuwa wametangaza kupiga marufuku maandamano hayo, wakishutumu chama hicho kwa kupanga maandamano yenye vurugu.

Kukamatwa kwa watu hao kulikuja licha ya Rais Samia Suluhu Hassan mnamo Januari 2023 kubatilisha marufuku ya mikusanyiko ya upinzani.

TRT Afrika