vijana wanaoandaman anchini Kenya wanasema hawana kiongozi wala uhusiano wowote na chama cha kisiasa au kabila,/ Picha : REeuters 

Hamasa zimeendelea kujitokeza mtandaoni huku kizazi cha Gen Z kinachoongoza maandamano dhidi ya serikali nchini Kenya kikichapisha orodha ya matakwa 10 wanayoitisha kutimizwa na serikali.

Vijana hao walianza maandamano yao kupinga mswada wa fedha 2024 kuanzia Juni 18 lakini licha ya Rais William Ruto kuridhia na kutangaza kuondoa mswada huo, bado vijana hao wamesisitiza kuendelea na maandamano huku wakimtaka Rais kujiuzulu.

Licha ya yote, vijana hao wanasema hawana kiongozi wala uhusiano wowote na chama cha kisiasa au kabila, na kuwa wanapigania haki ya vizazi vichanga na vijavyo.

Msimamo mkali

Orodha, imetokeza mtandaoni (ambayo haijathibitishwa chanzo chake) ikionyesha matakwa 10 wanayodai lazima yatimizwe na Rais Ruto kabla ya kutuliza hasira zao.

Pia wametaka serikali ichapishe maelezo ya namna fedha zote za serikali zilitumika katika kipindi cha mwaka 2023.

Miongoni mwa mambo makuu yanayodaiwa ni Kutii maagizo yote ya mahakama, kufuta ufadhili wa ofisi ya mke wa rais na mke wa naibu rais na kupunguzwa mishahara ya wabunge kutozidi shilingi 200 000 za Kenya.

Vijana hao wamadai kuwa fedha hizo badala yake zitumike kulipa mishahara ya walimu na madaktari.

Orodha hiyo ambayo imechapishwa na watu wengi wakiwemo baadhi ya wanasiasa katika mtandao wa X pia imeitisha kuondolewa ushuru wa nyumba na kurejeshwa fedha zilizotozwa kwa wafanyakazi kuelekea hilo.

Pia wametaka serikali ichapishe maelezo ya namna fedha zote za serikali zilitumika katika kipindi cha mwaka 2023.

Japo hakuna thibitisho orodha hiyo imetolewa na nani au uhakiki wake, imeendelea kusambazwa mtandaoni.

Taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya Rais ambayo pia ilichapishwa mtandaoni ilikuwa imeelezea awali kuwa serikali inataka kufanya mazungumzo na vijana kuangazia masaibu yote walioyotaja na kutafuta suluhu ya kudumu.

TRT Afrika